Simbu Ateka Mitaa ya Jiji la Dar es Salaam

September 24, 2025


WhatsApp%20Image%202025-09-23%20at%2019.48.18

WhatsApp%20Image%202025-09-23%20at%2019.48.19

WhatsApp%20Image%202025-09-23%20at%2019.48.22

WhatsApp%20Image%202025-09-23%20at%2019.48.25

WhatsApp%20Image%202025-09-23%20at%2019.48.25%20(1)

WhatsApp%20Image%202025-09-23%20at%2019.48.17


Na Tullo Chambo, Riadha Tanzania.

MWANARIADHA wa Kimataifa wa Tanzania, Bingwa wa Dunia Marathon,   Sajenti Alphonce Simbu, amekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam, mara aliporejea nchini akitokea Tokyo Japan.

Simbu, Septemba 16 mwaka huu, aliandika historia baada ya kuibuka Bingwa wa Dunia Marathon akitumia saa 2:09:48.03 katika Mashindano ya Dunia 'World Athletics Championship 2025 Tokyo Japan na kuwa Mtanzania wa kwanza kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano hayo makubwa kabisa duniani.

Simbu akiambatana na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Rogath John na Kocha Denis Malle,  alirejea nchini alfajiri ya Septemba 23  na kupata mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha sambamba na Naibu Mkurugenzi wa Michezo Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Penina Igwe.

Mara baada kuwasili, Simbu alipata mapumziko katika hoteli ya Blue Saphire Vingunguti na majira ya saa 4 asubuhi akiwa katika gari maalumu na msafara wa magari kadhaa ukiongozwa na Polisi wa Jeshi (MP), ulizunguka katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam na kupita maeneo ya Karume, Kariakoo (Mzunguko wa Msimbazi), Mnazi Mmoja, Posta Mpya, Bandarini hadi hoteli ya Tiffany Diamond.

Simbu akiwa na medali yake ya dhahabu, akiwa juu ya gari akiwapungia wananchi waliokuwa pembezoni mwa barabara ambao walikuwa wamejaa shangwehuku wengine wakipigana vikumbo kumshika mkono na wengine kupiga naye picha huku wakimpongeza.

Kufika barabara ya Morogoro  msafara wa Simbu ulipita mbele ya Shule ya Msingi Mtendeni ambapo wanafunzi walishindwa kujizuia na kupanda ukuta ili kumshuhudia.

Kivutio kingine alikuwa mwananchi mmoja mlemavu wa miguu, ambaye alikuwa amepandwa na hisia kali akitamani naye kumshika mkono Simbu, lakini akawa anashindwa kumfikia juu ya gari, kabla msamaria mmoja kumnyanyua na hatimaye kufanikisha azma yake ya kusalimiana na Bingwa huyo wa Dunia kwa staili ya kugonga naye 'tano'.

Msafara huo wa Simbu, pia ulipambwa na burudani ya matarumbeta kutoka kikundi cha Jeshi, ambacho kilikuwa burudani ya aina yake.
Hafla maalumu ya Simbu, inatarajiwa kufanyika Septemba 27 mwaka huu.

Joseph Panga Apokelewa na Viongozi wa Mkoa wa Arusha

September 23, 2025

 

Mwanariadha Joseph T. Panga apokelewa na Viongozi waandamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mkoa wa Arusha Babu Gerald (Mwenye Koti la Suti) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro baada ya kushika nafasi ya tisa kwa muda wa saa mbili , dakika tisa na sekunde thelathini na tano (2:09:35) katika mashindano ya Berlin Marathon 2025




Simbu takes Tanzania's first global title with marathon victory in Tokyo

September 15, 2025

 







Alphonce Felix Simbu made history on Monday (15), becoming the first athlete from Tanzania to win a global title by claiming gold in the men's marathon at the World Athletics Championships Tokyo 25.

He achieved the feat in style – with the smallest winning margin ever in a global championships marathon, having outsprinted Germany's Amanol Petros in the closing stages to finish just 0.03 ahead.

One of only two athletes representing Tanzania at the World Championships, Simbu was always in contention. He kicked in the closing 30 metres and with victory, he upgraded the world bronze medal he won in 2017 to gold.

“Today means celebrations in Tanzania,” he said. “We have written new history as a country. It was my dream. I am at peace. It is about discipline, training and never giving up.

“After 2017 I have been trying to win another medal but failed at it. Last year Paris was a challenge and this year I told myself: I will try my best. I did different types of training under different weather conditions.”

Simbu and Petros were both credited with the same time: 2:09:48.

“I have never seen something like this in the marathon – both races (men and women) came down to a sprint finish. It's like the 100m,” said Petros.

“This is four months of hard work in training – running, eating and sleeping. It was hard. But this silver gives me energy and bigger motivation that I can win bigger competitions. I was so sure I was winning, he (Simbu) surprised me. He kicked like crazy. I accept I lost today but tomorrow I can win. Today is a learning experience.”

Italy’s Iliass Aouani took bronze in 2:09:53.

“I am proud and happy about the way I conducted the race,” he said. “I was relaxed at the end and pushed through, but the other guys had more legs than me. It means a lot. This is a hard sport, people do not know that behind this medal are a lot of frustrations, a lot of bad races, missed opportunities.”

Kenya’s Vincent Ngetich took an early lead, with all the athletes grouped together. He led through 5km in 15:22, followed closely by athletes including Petros, Simbu and Aouani, plus Abel Chelangat, Isaac Mpofu, Sondre Moen, Suldan Hassan, Deresa Geleta and Stephen Kissa.

In the hot and humid conditions, athletes cooled themselves with ice and sponges, even passing them to each other.

Ngetich, running on the edge of the course, slightly increased the pace, with Chelangat and Kissa close behind. The leading pack briefly scattered before regrouping.

At Akihabara turn, Ngetich pushed the pace again, but Germany’s Richard Ringer took over and led the group through 10km in 30:48, alongside defending champion Victor Kiplangat, Chelangat, Petros, Simbu, Ngetich and Mohamed Reda El Aaraby. 

The leading roles kept changing, with Morocco’s El Aaraby taking over before Ethiopia’s Tadese Takele – this year’s Tokyo Marathon champion – surged ahead. Ngetich again took the lead through the Ginza turn.

Kiplangat then grabbed a cooler and moved to the front, pushing the pace downhill. Sweden’s Hassan led a group of more than 20 runners through 20km in 1:01:54 but Kiplangat remained in control at the halfway point (1:05:19), followed by the likes of Hassan, Geleta, Kissa, Elroy Gelant and Kipkoech.

Geleta took a turn at the front, leading the pack through 30km in 1:32:27, but it was Kiplangat who surged at 33km – leading for around 6km before falling back and out of contention.

Meanwhile, his compatriot Chelangat took the lead, followed by a series of challengers – all in single file. Soon, the lead group was down to five.

As the race wound up, Chelangat and Haimro Alame dropped back, leaving Aouani, Petros and Simbu to battle for the gold. With the stadium in sight, Simbu nearly went off course.

Once inside, Petros surged with 200 metres to go, with Simbu in pursuit. Petros glanced back twice and the world title came down to a photo finish. Both were timed at 2:09:48, separated by just three hundredths of a second.

“When we entered the stadium, I was not sure if I would win. I did not know if I won. But when I saw the video screens and me on the top of the results, I felt relieved,” said Simbu.

“Before this event, I was training in Tanzania, and the conditions there helped me to win this race. I remember, when I was in Paris last year (at the Olympics), it was very challenging for me – the hills, all ups and downs. So, before Tokyo, I decided to train on different surfaces. Sometimes I went to hills, and that is what made the difference here. I had many tough moments during the race, but I told myself that I would never give up.”

Credit : Michelle Katami for World Athletics

Alphonce Felix Simbu is Ready for World Championships Tokyo 2025

September 14, 2025

 


The Kit for Alphonce Felix Simbu, Ready for the Race, World Athletics Championships Tokyo 2025 Japan,  Sponsored by Xtep Gears

Simbu , Gisemo Kuipeperusha Bendera ya Tanzania Tokyo Japan.

September 14, 2025

 

Wanariadha wa Kimataifa , Alphonce Felix Simbu na Josephat Joshua Gisemo kuipeperusha Bendera ya Tanzania leo Usiku kwenye Mashindano ya Dunia (World Championships 2025) ya Riadha huko Tokyo Japan.

Bofya Hapa kwa Maelezo Zaidi

 

Copyright © 2015 - 2025 Athletics Tanzania All Right Reserved

Developed by Gadiola Emanuel
Theme By AP | Developed By Gadiola Emanuel