Walemavu
wakishangilia kwa pamoja na viongozi wa kampuni ya GAPCO ambao walikuwa
ndiyo wadhamini mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016
zilizofanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Walemavu
wakianza kutimua mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016
zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini
Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Viongozi
wa kampuni ya GAPCO wakiwa na Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili toka kushoto) akiwaangalia
walemavu wakitimua mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016
zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini
Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja
ya walemavu Vosta Peter (30) kutokea Dar es Salam akiongoza katika mbio
za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa
na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Kila mmoja akionyesha ustadi wa kuendesha baskeli.
Mwanadada
Linda Macha (32) ambaye aliweza kuwashinda wenzake katika mbio za
Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na
kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mshindi
wa mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016, Vosta Peter (30)
akishangilia mara baada ya kumaliza. Mbio hizo za Kilometa 10
zilidhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mshindi
wa kwanza kwa mbio za walemavu kilomita 10, Vosta Peter (30) akipokea
cheki ya Shilingi Milioni Moja kutoka kwa kampuni ya GAPCO,
wanaomkabidhi ni Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya (kushoto),
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu
(anayepiga makofi toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO
Tanzania, Vijay Nair.
Picha zote na Cathbert wa Kajunason Blog.
Na Cathbert Kajuna - Kilimanjaro.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya GAPCO Afrika Mashariki, Macharia Irungu amewataka
wanamichezo kujibidishe kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili waweze
kufanya vizuri katika mashindano wanayoshiriki.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki mjini Kilimanjaro wakati wa Mashindano ya Kilimanjaro
Marathoni 2016, ambapo GAPCO ndiyo waliodhamini upande wa Walemavu,
alisema kuwa wanamichezo wengi walemavu na hata wasiowalemavu hujisahau
sana kufanya mazoezi ya kutosha jambo linalowafanya wengi wao kutoweza
kufanikiwa kushinda kwenye mashindano.
Aliongeza
kuwa wao kampuni ya GAPCO waliweza kujitolea kuwasaidia walemavu ili
waweze kuonyesha vipaji vyao japo mwanzo waliweza kuwasisitiza wafanye
mazoezi na ndiyo maana wameweza kufanya vyema. "Napenda kuwaasa
wanamichezo wale walemavu na wasio walemavu, wapende kujitoa kufanya
mazoezi ya kutosha maana siri ya ushindi ni mazoezi wala hakuna muujiza
unaoweza kukupa ushindi kama haujajitoa kufanya mazoezi ya kutosha,"
alisema Irungu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Vijay Nair
alisema wamefurahishwa na mahudhurio ya watu wenye ulemavu waliojitoa
kushiriki mashindano hayo, na wao hawatawatupa wataendelea kuwa nao bega
kwa bega. Bw. Nair aliwaasa walemavu wawe na moyo wa upendo na
mshikamano ili waonyeshe mfano bora hata wanapojitokeza kusaidiwa
wafaidike kwa pamoja.
Mashindano
ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu zilidhaminiwa na
GAPCO ambapo shindano lilijumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi
matatu zenye viwango vya kimataifa wapatao 60 kutoka Dar es Salaam,
Arusha, Moshi na Zanzibar.
0 Comments