Showing posts with label News. Show all posts
Showing posts with label News. Show all posts

Dkt. Mwigulu Nchemba Aongoza Washiriki Zaidi ya 13,000 NBC Dodoma Marathon

July 28, 2026


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, leo ameongoza zaidi ya washiriki 13,000 katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2026 zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, huku akiipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kufanikisha ukusanyaji wa shilingi bilioni 1 zitakazotumika kuokoa maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia miradi ya afya ya mama na mtoto.

Fedha hizo zitasaidia utekelezaji wa maeneo matatu muhimu ya kijamii ambayo ni kupunguza vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua, kugharamia upasuaji wa watoto wenye matatizo ya moyo, pamoja na kuimarisha huduma za upandikizaji wa uloto kwa watoto wanaoishi na ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell).

Mbio hizo, ambazo zimeendelea kujijengea hadhi kama moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo nchini, zilihusisha washiriki kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali, huku zikishuhudia ushindani mkubwa kati ya wanariadha wa Tanzania na Kenya katika mbio za kilomita 21 na 42. Dkt. Nchemba, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi na sekta binafsi, walishiriki mbio za kilomita tano (5) kuhamasisha mazoezi na maisha yenye afya.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi na wadau wa mbio hizo, Dkt. Nchemba alisema mafanikio ya NBC Dodoma Marathon yanaonesha jinsi ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi unavyoweza kuleta matokeo yenye manufaa makubwa kwa jamii.

Alisema ongezeko la washiriki kutoka 1,500 mwaka 2020 hadi zaidi ya 13,000 mwaka 2026 ni ushahidi wa mwamko mkubwa wa Watanzania katika kushiriki michezo, kuzingatia afya zao na kuunga mkono shughuli za maendeleo kupitia michezo.

"NBC Dodoma Marathon imekuwa zaidi ya mashindano ya riadha. Leo ni jukwaa linalounganisha Watanzania na marafiki kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo la kufanya jambo kubwa zaidi—kuokoa maisha. Nawahimiza Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na figo," alisema Dkt. Nchemba.

Aidha alisema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Jiji la Dodoma kwa kupanua na kuboresha barabara muhimu, hatua itakayorahisisha shughuli za usafirishaji na wakati huo huo kuongeza usalama wa washiriki wa mbio hizo katika miaka ijayo.

Waziri Mkuu pia aliutaka uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuendelea kuziunga mkono mbio hizo kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa jiji hilo kupitia ongezeko la wageni, shughuli za utalii wa ndani, biashara za hoteli, migahawa, usafiri na huduma nyingine zinazochochewa na tukio hilo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule, alisema NBC Dodoma Marathon imeendelea kuwa kichocheo muhimu cha uchumi wa mkoa huo kwa kuongeza mzunguko wa fedha na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kila mwaka.

Aliishukuru Benki ya NBC kwa kuendelea kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo ya Mkoa wa Dodoma kupitia uwekezaji wake katika afya, michezo na maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi, alisema mafanikio ya mbio hizo yanaakisi dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kutumia biashara kama chachu ya kuleta maendeleo ya kijamii.

Alisema kati ya fedha zilizokusanywa, shilingi milioni 600 zimeelekezwa moja kwa moja katika utekelezaji wa malengo makuu ya NBC Dodoma Marathon kupitia taasisi tatu zinazotoa huduma muhimu za afya nchini.

Katika hafla hiyo, Dkt. Nchemba na Bw. Sabi walikabidhi hundi za misaada ambapo: Shilingi milioni 200 zilikabidhiwa Taasisi ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya kupanua programu ya ufadhili wa wakunga ili kuboresha huduma za afya ya uzazi, Shilingi milioni 200 zilikabidhiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kugharamia upasuaji wa watoto wenye matatizo ya moyo na Shilingi milioni 200 zilikabidhiwa Hospitali ya Benjamin Mkapa kusaidia huduma za upandikizaji wa uloto kwa watoto wenye ugonjwa wa selimundu.

"Mafanikio haya yanatokana na dhamira yetu ya kuhakikisha mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na ustawi wa jamii. Tunawashukuru washiriki wote, wadhamini na wadau mbalimbali waliochangia kufanikisha NBC Dodoma Marathon 2026. Ushirikiano huu umewezesha kuokoa maisha ya Watanzania wengi," alisema Bw. Sabi.

Alitoa shukrani maalumu kwa wadhamini wakuu wa mbio hizo akiwemo Sanlam Allianz, GSM Group, Vodacom Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na wadau wengine waliochangia mafanikio ya tukio hilo.

Katika mbio za kilomita 42 (Full Marathon) kwa upande wa wanaume, mwanariadha kutoka Kenya Edwin Koech aliibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia muda wa saa 2:05:12, akifuatiwa na Vitalis Kibiwott aliyemaliza kwa saa 2:12:18.

Kwa upande wa wanawake, Agnes Ngolo wa Kenya alitwaa ushindi kwa kutumia muda wa saa 2:32:36, huku Jacinta Chepkoech, pia kutoka Kenya, akimaliza wa pili kwa muda wa saa 2:33:26.

Washindi wa nafasi ya kwanza hadi ya kumi walizawadiwa fedha taslimu, ambapo washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake kila mmoja alijishindia Tsh milioni 11.5.

Katika mbio za kilomita 21 (Half Marathon) kwa wanaume, Bernard Geay wa Tanzania aliibuka mshindi wa kwanza kwa muda wa saa 1:02:46, akifuatiwa na Simon Kelenzoke wa Kenya (1:02:57), huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Michael Geay wa Tanzania kwa muda wa 1:02:59.

Kwa upande wa wanawake, Magdalena Shauri wa Tanzania aliibuka mshindi wa kwanza kwa muda wa 1:08:59, akifuatiwa na Doreen Chetzop wa Kenya aliyemaliza kwa muda wa 1:10:36.

Washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake walijishindia Tsh milioni 5.5, huku washindi wa pili wakiondoka na Tsh milioni 2.5.

NBC Dodoma Marathon imeendelea kuthibitisha kuwa si tu tamasha kubwa la michezo nchini, bali pia ni jukwaa la kuhamasisha afya, kuunganisha jamii, kukuza uchumi wa Jiji la Dodoma na kuchangia moja kwa moja kuboresha huduma muhimu za afya kwa Watanzania.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh milioni 200 kwa muwakilishi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) (wanne kushoto) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa ajili ya kugharamia upasuaji wa watoto wenye matatizo ya moyo kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa nne kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya NBC , Dkt. Elirehema Doriye (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa SanlamAllianz, wadhamini wakuu wa mbio hizo, Bw Julius Magabe (kushoto) na viongozi wengine kutoka serikalini na wadau wa mbio hizo.




Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh milioni 200 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Profesa Abel Makubi (wa tatu kushoto) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa ajili ya kusaidia huduma za upandikizaji wa uloto kwa watoto wenye ugonjwa wa selimundu (sicke cell)kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Dkt. Elirehema Doriye (kushoto) na viongozi wengine kutoka serikalini na wadau wa mbio hizo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh milioni 200 kwa muwakilishi wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation (wanne kushoto) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa ajili ya kwa ajili ya kupanua programu ya ufadhili wa wakunga ili kuboresha huduma za afya ya uzazi kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa nne kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya NBC , Dkt. Elirehema Doriye (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa SanlamAllianz, wadhamini wakuu wa mbio hizo, Bw Julius Magabe (kushoto) na viongozi wengine kutoka serikalini na wadau wa mbio hizo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, (wa tatu kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh mil 5.5 kwa mwanariadha kutoka Tanzania, Magdalena Shauri alieibuka mshindi wa kwanza (kwa upande wa wanawake) wa mbio za km 21 za NBC Dodoma Marathon, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kulia) na viongozi wengine kutoka serikalini na wadau wa mbio hizo.



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh mil 11.5 kwa mwanariadha kutoka Kenya, Edwin Koech alieibuka mshindi wa kwanza (kwa upande wa wanaume) wa mbio za km 42 za NBC Dodoma Marathon, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia)

Goal Setting & Training Strategies and Mental Toughness Techniques.

December 15, 2025

 









🎯 I. Goal Setting & Training Strategies

The best way to maintain long-term motivation is to ensure your training remains purposeful, fun, and varied.

1. Set SMART Goals (Short-Term & Long-Term)

  • Long-Term Goals: These are your ultimate aspirations (e.g., qualifying for a championship, setting a school record, or achieving a specific personal best like $10.5$ seconds in the 100m).

  • Short-Term Goals: Break down the big goal into daily, weekly, and monthly milestones. These provide constant small wins and immediate purpose.

    • Example: Improving a specific phase of your race (e.g., "reduce time to 10m by $0.05$ seconds"), executing a technical drill perfectly, or consistently hitting a certain weight in the weight room.

  • Track Your Progress: Keep a log of your workouts, times, and how you felt. Seeing tangible proof of your strength and speed gains is a massive psychological boost.

2. Introduce Variety and Fun

  • Avoid the Rut: Repetitive training is a major cause of burnout. Mix up your training with new routes, different types of drills, or even a complementary sport (like swimming or cycling) to keep the body and mind fresh.

  • Training Partners/Group: Training with a partner or group provides social motivation and accountability. It's much harder to skip a practice when someone is relying on you to show up.

  • Reward Milestones: Celebrate small achievements. This could be a new pair of shoes after a successful training block, a favorite meal after a tough workout, or a dedicated rest day.

3. Prioritize Recovery

Overtraining leads to fatigue, injury, and a rapid drop in motivation.

  • Sleep: Aim for 8–10 hours of sleep per night. This is when your body repairs and your muscles strengthen.

  • Active Rest: Incorporate true rest days and lower-intensity activities like yoga or dynamic stretching to aid recovery.


🧠 II. Mental Toughness Techniques

In track and field, your mind is often the first thing to quit. Building mental resilience is as important as building physical strength.

1. Visualization (Mental Rehearsal)

  • Take time before a race or practice to mentally rehearse a perfect performance.

  • See the start gun, feel your body's movements, hear the crowd, and experience the feeling of achieving your goal. This primes your mind and body for success, reducing anxiety on race day.

2. Positive Self-Talk

  • Replace negative thoughts with actionable, positive affirmations.

    • Instead of: "I'm so tired, I can't finish this."

    • Think: "I am strong. I prepared for this. Finish the last rep with great form."

  • Develop a Mantra: Use a short phrase to refocus when pain or doubt creeps in (e.g., "Push through," "Relentless," "One more").

3. Embrace the Struggle (The "Growth Mindset")

  • Redefine Failure: View missed marks or poor times not as a definition of your ability, but as feedback on what needs to be adjusted in training.

  • Focus on Effort over Outcome: Remind yourself that the effort and discipline you show today are what truly build strength for tomorrow.

    • As legendary runner Steve Prefontaine said: “A lot of people run a race to see who is fastest. I run to see who has the most guts.”

4. Stay Present ("In the Zone")

  • Focus only on the immediate task: the next step, the next throw, or the next hurdle.

  • Block out uncontrollable factors like weather, competitors, or past mistakes. Elite athletes focus on a state of "flow" where they are totally immersed in the action.

Benjamin Ferdinandi Ratsim Avunja Rekodi ya Taifa Kilomita 15

November 24, 2025

 

Mwanariadha Benjamin Fernandi Ratsim  Apokelewa na Rais wa shirikisho la Riadha Tanzania -RT Rogath John Stephen Akhwari (Kushoto) na Kocha Dennis Malle (Kulia) baada ya kushinda medali ya shaba katika mbio za kilomita 15 @nnzevenheuvelenloop kwa Dakika 41:49 na kuvunja rekodi ya Taifa huko Uholanzi. #AthleticsTanzania 



Finalists announced for 2025 Athlete of the Year awards

November 22, 2025

 

The 12 Athlete of the Year finalists have been confirmed, as the countdown to the World Athletics Awards 2025 continues.

The top two athletes in each category – track, field and out of stadium – have been chosen from the first round of voting, which comprised votes from the World Athletics Council, World Athletics Family and a public vote on social media. One of the two athletes will take the crown in their category.

A final round of voting – cast by fans of the sport – will now take place between 4-9 November to help select the overall women’s and men’s World Athlete of the Year.

Vote now


Finalists

Women’s track athlete of the year
Femke Bol (NED) – world 400m hurdles champion
Sydney McLaughlin-Levrone (USA) – world 400m champion

Men’s track athlete of the year
Noah Lyles (USA) – world 200m champion
Emmanuel Wanyonyi (KEN) – world 800m champion

Women’s field athlete of the year
Tara Davis-Woodhall (USA) – world long jump champion
Nicola Olyslagers (AUS) – world high jump champion

Men’s field athlete of the year
Mondo Duplantis (SWE) – world pole vault champion
Mattia Furlani (ITA) – world long jump champion

Women’s out of stadium athlete of the year
Peres Jepchirchir (KEN) – world marathon champion
Maria Perez (ESP) – world 20km and 35km race walk champion

Men’s out of stadium athlete of the year
Sabastian Sawe (KEN) – London Marathon and Berlin Marathon champion
Alphonce Simbu (TAN) – world marathon champion

The Athletes of the Year in each category, as well as the overall winners, will be revealed at a ceremony in Monaco on Sunday 30 November as part of the World Athletics Awards 2025.

World Athletics


🏆 Vote for the Finish That Made History! Alphonce Simbu: World Athletics Out of Stadium Athlete of the Year

November 09, 2025

 

In a moment so dramatic it redefined endurance running, Alphonce Simbu delivered a finish for the ages at the Tokyo World Championships.

After 42.195 grueling kilometers, the men's marathon came down to a breathtaking sprint inside the National Stadium.

  • The Race: A tactical masterclass through the streets of Tokyo.

  • The Moment: A stunning, last-second surge and a full-body lunge across the line.

  • The Verdict: A photo finish confirmed it—Alphonce Simbu won Tanzania's first-ever World Championship gold medal by the closest margin in history: a mere 0.03 seconds!

This was the ultimate test of heart, kick, and grit, crowning Simbu the undisputed World Marathon Champion.

Now, he's a nominee for the prestigious World Athletics Out of Stadium Athlete of the Year award.

A marathon decided like a 100m sprint! His historic victory against German Amanal Petros is a testament to unwavering determination that deserves the world's highest honor.

Your Vote Counts! Help celebrate this incredible, history-making moment! Cast your vote for the man who proved that in the marathon, the last three hundredths of a second are all that matters.

#VoteSimbu #WorldChampion #OutOfStadiumAOY #AthleticsAwards





Alphonce Felix Simbu Kuwania Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Dunia (Alphonce Simbu for World Athletics Men's Out of Stadium Athlete of the Year!)

November 09, 2025

 

The 12 Athlete of the Year finalists have been confirmed, as the countdown to the World Athletics Awards 2025 continues.

The top two athletes in each category – track, field and out of stadium – have been chosen from the first round of voting, which comprised votes from the World Athletics Council, World Athletics Family and a public vote on social media. One of the two athletes will take the crown in their category.

A final round of voting – cast by fans of the sport – will now take place between 4-9 November to help select the overall women’s and men’s World Athlete of the Year.

Vote now


Finalists

Women’s track athlete of the year
Femke Bol (NED) – world 400m hurdles champion
Sydney McLaughlin-Levrone (USA) – world 400m champion

Men’s track athlete of the year
Noah Lyles (USA) – world 200m champion
Emmanuel Wanyonyi (KEN) – world 800m champion

Women’s field athlete of the year
Tara Davis-Woodhall (USA) – world long jump champion
Nicola Olyslagers (AUS) – world high jump champion

Men’s field athlete of the year
Mondo Duplantis (SWE) – world pole vault champion
Mattia Furlani (ITA) – world long jump champion

Women’s out of stadium athlete of the year
Peres Jepchirchir (KEN) – world marathon champion
Maria Perez (ESP) – world 20km and 35km race walk champion

Men’s out of stadium athlete of the year
Sabastian Sawe (KEN) – London Marathon and Berlin Marathon champion
Alphonce Simbu (TAN) – world marathon champion

The Athletes of the Year in each category, as well as the overall winners, will be revealed at a ceremony in Monaco on Sunday 30 November as part of the World Athletics Awards 2025.

World Athletics





This year, Alphonce Simbu delivered a performance for the history books!

🇹🇿 Make History with Tanzania's Marathon Champion! 🇹🇿

His season highlight was a breathtaking, photo-finish victory in the World Marathon Championships in Tokyo, securing Tanzania's first-ever gold medal at a World Athletics Championships! A true display of grit, endurance, and a final, unforgettable kick.


His Achievements Speak for Themselves:

  • 🥇 World Marathon Champion (Tokyo 2025)

  • 🥈 Boston Marathon Runner-up

  • A Season of Relentless Endurance

He is a finalist for the prestigious World Athletics Men's Out of Stadium Athlete of the Year award. This is the time to honor his journey and remarkable 2025 season!


Your Vote Matters!

Help crown the champion who brought home historic gold!

How to Vote: The final round of fan voting for the overall World Athlete of the Year (which includes all category winners) is open!

  • Visit the World Athletics official voting channels (check their website or social media platforms like Facebook, X/Twitter, or Instagram for the link).

  • Cast your vote for Alphonce Simbu!

Voting deadline is imminent! Don't miss your chance to support a legend!

#VoteSimbu #WorldAthleticsAwards #MarathonKing #Tanzania


Simbu takes Tanzania's first global title with marathon victory in Tokyo

September 15, 2025

 







Alphonce Felix Simbu made history on Monday (15), becoming the first athlete from Tanzania to win a global title by claiming gold in the men's marathon at the World Athletics Championships Tokyo 25.

He achieved the feat in style – with the smallest winning margin ever in a global championships marathon, having outsprinted Germany's Amanol Petros in the closing stages to finish just 0.03 ahead.

One of only two athletes representing Tanzania at the World Championships, Simbu was always in contention. He kicked in the closing 30 metres and with victory, he upgraded the world bronze medal he won in 2017 to gold.

“Today means celebrations in Tanzania,” he said. “We have written new history as a country. It was my dream. I am at peace. It is about discipline, training and never giving up.

“After 2017 I have been trying to win another medal but failed at it. Last year Paris was a challenge and this year I told myself: I will try my best. I did different types of training under different weather conditions.”

Simbu and Petros were both credited with the same time: 2:09:48.

“I have never seen something like this in the marathon – both races (men and women) came down to a sprint finish. It's like the 100m,” said Petros.

“This is four months of hard work in training – running, eating and sleeping. It was hard. But this silver gives me energy and bigger motivation that I can win bigger competitions. I was so sure I was winning, he (Simbu) surprised me. He kicked like crazy. I accept I lost today but tomorrow I can win. Today is a learning experience.”

Italy’s Iliass Aouani took bronze in 2:09:53.

“I am proud and happy about the way I conducted the race,” he said. “I was relaxed at the end and pushed through, but the other guys had more legs than me. It means a lot. This is a hard sport, people do not know that behind this medal are a lot of frustrations, a lot of bad races, missed opportunities.”

Kenya’s Vincent Ngetich took an early lead, with all the athletes grouped together. He led through 5km in 15:22, followed closely by athletes including Petros, Simbu and Aouani, plus Abel Chelangat, Isaac Mpofu, Sondre Moen, Suldan Hassan, Deresa Geleta and Stephen Kissa.

In the hot and humid conditions, athletes cooled themselves with ice and sponges, even passing them to each other.

Ngetich, running on the edge of the course, slightly increased the pace, with Chelangat and Kissa close behind. The leading pack briefly scattered before regrouping.

At Akihabara turn, Ngetich pushed the pace again, but Germany’s Richard Ringer took over and led the group through 10km in 30:48, alongside defending champion Victor Kiplangat, Chelangat, Petros, Simbu, Ngetich and Mohamed Reda El Aaraby. 

The leading roles kept changing, with Morocco’s El Aaraby taking over before Ethiopia’s Tadese Takele – this year’s Tokyo Marathon champion – surged ahead. Ngetich again took the lead through the Ginza turn.

Kiplangat then grabbed a cooler and moved to the front, pushing the pace downhill. Sweden’s Hassan led a group of more than 20 runners through 20km in 1:01:54 but Kiplangat remained in control at the halfway point (1:05:19), followed by the likes of Hassan, Geleta, Kissa, Elroy Gelant and Kipkoech.

Geleta took a turn at the front, leading the pack through 30km in 1:32:27, but it was Kiplangat who surged at 33km – leading for around 6km before falling back and out of contention.

Meanwhile, his compatriot Chelangat took the lead, followed by a series of challengers – all in single file. Soon, the lead group was down to five.

As the race wound up, Chelangat and Haimro Alame dropped back, leaving Aouani, Petros and Simbu to battle for the gold. With the stadium in sight, Simbu nearly went off course.

Once inside, Petros surged with 200 metres to go, with Simbu in pursuit. Petros glanced back twice and the world title came down to a photo finish. Both were timed at 2:09:48, separated by just three hundredths of a second.

“When we entered the stadium, I was not sure if I would win. I did not know if I won. But when I saw the video screens and me on the top of the results, I felt relieved,” said Simbu.

“Before this event, I was training in Tanzania, and the conditions there helped me to win this race. I remember, when I was in Paris last year (at the Olympics), it was very challenging for me – the hills, all ups and downs. So, before Tokyo, I decided to train on different surfaces. Sometimes I went to hills, and that is what made the difference here. I had many tough moments during the race, but I told myself that I would never give up.”

Credit : Michelle Katami for World Athletics

Alphonce Felix Simbu is Ready for World Championships Tokyo 2025

September 14, 2025

 


The Kit for Alphonce Felix Simbu, Ready for the Race, World Athletics Championships Tokyo 2025 Japan,  Sponsored by Xtep Gears

Simbu , Gisemo Kuipeperusha Bendera ya Tanzania Tokyo Japan.

September 14, 2025

 

Wanariadha wa Kimataifa , Alphonce Felix Simbu na Josephat Joshua Gisemo kuipeperusha Bendera ya Tanzania leo Usiku kwenye Mashindano ya Dunia (World Championships 2025) ya Riadha huko Tokyo Japan.

Bofya Hapa kwa Maelezo Zaidi

RT Kuwabana Waandaaji wa Mbio

August 20, 2025


WhatsApp%20Image%202025-08-20%20at%2015.09.17


SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) limepanga kuweka sheria mpya itakayowalazimisha wandaaji wa mashindano kuhakikisha wanajumuisha pia mbio za watoto katika kila tukio litakaloandaliwa.


Hatua hiyo inalenga kujenga msingi imara wa vipaji na kuwekeza mapema kwenye maendeleo ya riadha nchini.


Rais mpya wa RT, Rogath John Stephen Akhwari, alisema mpango huo utahusisha kuandaa mashindano maalumu ya watoto na vijana kwa kila kanda, yakiratibiwa kwa kushirikiana na vyama vya mikoa ili kuhakikisha kunakuwepo mtiririko wa mashindano kuanzia ngazi ya chini.


Akhwari alibainisha kuwa wapo mbioni kuandaa kanuni mpya za kusimamia mbio za barabarani, ambapo kutakuwa na utaratibu wa kutofautisha mashindano ya kimaifa yatakayosimamiwa na RT moja kwa moja na yale ya ndani yenye malengo ya kitaifa, kwa lengo la kuongeza ubora na hadhi ya riadha nchini.


“Hizi mbio itakuwa ni lazima, siyo chaguo tunataka kuboresha kanuni zetu na yeyote atakayehitaji kibali cha kuandaa mashindano atalazimika kuhakikisha mbio za watoto pia zitakuwepo,” alisema Akhwari.


Alieleza watapeleka wataalamu waliobobea ili kusaidia wandaaji kuelewa namna sahii ya kuandaa mashindano ya watoto, akisisitiza kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo awali ni watoto kukimbia mbio ndefu zisizolingana na umri wao.


"Watoto wetu wamekuwa wakikosa fursa hizi, kwa sababu mara nyingi wakipewa mbio wanakimbizwa umbali wa kilometa tano, hapo awali tulivumilia kwa sababu tulikuwa hatuna mfumo madhubuti lakini sasa tunataka kubadilisha hilo,” aliongeza.


Aidha kabla ya sheria mpya kupitishwa, RT imesema itatoa elimu kwa wandaaji wote wa mbio, kisha kuwapa muda wa maandalizi kabla ya utekelezaji rasmi.


Akhwari anasema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha riadha Tanzania inakua kwa kuanzia watoto, vijana hadi kuzalisha wanariadha wa kiwango cha kimataifa.


Imeandaliwa na Mwananchi Communications Limited

MAPOKEZI YA RAIS WA RT ROGATH JOHN STEPHEN AKHWARI JIJINI ARUSHA

August 18, 2025

 

Kocha Mwingereza akimpongeza rais wa shirkisho la Riadha Tanzania -RT Kocha Rogath John Stephen Akhwari wakati wa mapokezi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Leo.

Mke wa Rogath John (katikati mwenye jaketi jekundu) akimpongeza mume wake kwa kuchaguliwa kuwa rais wa shirikisho la Riadha Tanzania -RT wakati wa mapokezi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Leo.
Rais wa shirikisho la Riadha Tanzania -RT Kocha Rogath John Stephen Akhwari Akiwashukuru Watanzania wote kwa Kumuombea na hatimaye kuchaguliwa kuwa rais , pia amechukua nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake kwenye michezo.


Na John Mhala, Arusha.

ARUSHA: Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Rogath John Stephen Akhwari amesema safari ya kuendeleza mchezo wa riadha ndio imeanza kwani shirikisho hilo litaanzisha rasmi mbio za watoto na vijana lengo ni kuwatayarisha wenye umri huo kuwa kurithi mikoba ya wanariadha wanaojiandaa kustaafu.

Stephen amesema hayo leo alfajiri alipowasili jijini Arusha akitokea Mwanza baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa RT kuwa Rais wa Shirikisho hilo na kusema kuwa wakati umefika sasa wa kuwaandaa watoto na vijana kushiriki mchezo wa riadha ili waweze kushika nafasi za akina Alphonce Simbu ,Magdalena Shauri,Jackline Sakilu na Gabriel Geay watakapostaafu.

Amesema RT lazima ijiandae kwa kuwaanda watoto na vijana ili waupende mchezo huo na hatimaye waweze kufanya vizuri kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na kushika zile nafasi walizofanya vizuri wanariadha wenzao hivyo wale wote wanaoanzisha na walioanzisha mbio kote nchini kipaumbele ni kuanzisha mbio za watoto na vijana mara moja kwani ndio lengo la msingi la kukuza mchezo huo unapendwa kwa sasa hapa nchini.

Rais huyo amesema ajira kwa sasa ni ngumu iwe ndani ya serikali na nje ya serikali na ajira nzuri ni mchezo wa riadha hivyo aliwaasa wazazi kuwapa ushirikiano watoto na vijana kujikita katika mchezo huo kwani una pesa nyingi kwa muda mfupi na kutoa mfano Simbu aliposhinda mbio za Boston amepata fedha nyingi ambazo hata waziri akistaafu serikali hawezi kuzipata.

Rogath ambaye mwajiriwa wa jeshi la Polisi nchini na kituo chake cha kazi Polisi Kati Arusha kwa cheo cha Mrakibu Msaidizi Mwandamizi (ASP) alimshukuru sana Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Inspekta General wa Polisi, Camilius Wambura kwa kumpa baraka za kuchukua fomu za kuwania kinyang’anyanyiro hicho na hatimaye kushinda urais.

 

Copyright © 2015 - 2025 Athletics Tanzania All Right Reserved

Developed by Gadiola Emanuel
Theme By AP | Developed By Gadiola Emanuel