Home
Riadha
Watanzania watamba Ngorongoro Marathon 2015
Watanzania watamba Ngorongoro Marathon 2015
By
Athletics Tanzania
August 21, 2015
 |
Waziri mkuu Mstaafu , Fredrick Sumaye akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo
waandaji buda mfupi kabla ya kuanza kwa mbio za Km 21 Katika gate la
kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro, |
 |
Waziri mkuu Msaatfu Fredirick Sumaye
akikimbia sambamba na rais wa shirikisho la riadha Tanzania,RT,Athony
Mtaka(Kushoto kwake) mkuu wa mkoa wa Arusha ,Daud Ntibenda,pamoja na
mkuu wa wilaya ya Karatau Omary Kwaang kuashiria kuanza kwa mbio za
Ngorongoro Marathoni. |
 |
Maratibu wa Mbio , Meta Paul akiwa na mmoja
wa wasiamamizi ,Leila wakati wakiwaandaa wanariadha kuanza mbio za Km
21 katika lango la kuingilia hifadhi ya taifa ya
Ngorongoro. |
 |
Mbio zikianza rasmi. |
 |
Baaadhi ya washiriki katika mbio hizo
,walikuwemo pia wadhamini kama Maremga Investment,hapa Marenga mwenye
truck suit nyeusi akijaribu kukimbiza upepo. |
 |
Awawli mbio zikiwa bado ndio zimeanza kundi
la wakimbiaji lilionekana wote wanakimbia kwa karibu. |
 |
Muda ulivyosonga na hatua ndivyo zilivyo
ongezeka. |
 |
Hatimaye wakaanza kuachana mmoja baada ya
mmoja, |
 |
Wengine wakaamua kwenda pamoja ili kupeana
moja. |
 |
wengine wakafunguka zaidi. |
 |
Hatimaye wakapatikana wakimbiaji watatu
wakaongoza hadi mwisho wa mbio na hawa ni ,Joseph
Theofily(katikati),George Gerald (kulia) na Emanuel
Giniki. |
 |
Mkimbiaji raia wa Kenya ambaye jina lake
halikufahamika mara moja akijaribu kuonesha umahiri wake katika mbio
hizo. |
 |
Msichana pekee aliyekuwa akiongoza ni
Failuna Abdi . |
 |
Nyuma ya Failuna alikuwepo Nathalia
Elisante. |
 |
Mshindi wa kwanza katika Mbio za Ngorongoro
Maratahoni 2015 ,Joseph Theofily akimaliza mbio hizo katika uwanja wa
Mazingira Bora akitumia muda wa 1:03:09. |
 |
Mshindi wa Pili katika mbio hizo ,George
Gerald akihitimisha mbio hizo akitumia muda wa
1:03:36 |
 |
Mshindi wa tatu ,Emanuel Giniki
akikalimilisha mbio kwa muda wa 1:03:42. |
 |
Giniki akijaribu kupoza koo mara baada ya
kumaliza mbio. |
 |
Mkimbiaji wa klabu ya riadha ya
Holili,Osward Moris akihitimisha mbio. |
 |
Mshindi wa kwanza kwa kina dada Failuna Abdi
akihitimisha mbio katika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa 1
:10:25 |
 |
Mgeni rasmi katika mbio hizo ,Waziri mkuu
Mstaafu ,Fredirck Sumaye akiingia uwanjani huku akihitimisha mbio za
km 21 .
WANARIADHA wa
Tanzania Joseph Theofily wa klabu ya riadha ya Holili
ya mkoani Kilimanjaro na Failuna
Abdi wa klabu ya riadha ya Winning Spirit ya jijini Arusha wamefanikiwa kupeperusha
vyema Bendera ya taifa baada ya
kuibuka washindi wa kwanza katika mbio za kimataifa za Ngorongoro
Marathoni kwa upande wa wanaume na wanawake.
Mwanariadha Theofily alifanikiwa kumaliza mbio za
km 21 akitumia muda wa saa 1:03:09 na
kujinyakulia kitita cha sh Mil, 1. mbele ya wakongwe wengine kutoka nchi za Kenya ,Uganda na Malawi
huku Gabriely Gerald wa klabu ya
Winning Spirit ya jijini Arusha akishika nafasi ya
pili akimaliza mbio akitumia saa
1:03:36 na kujinyakulia kitita cha sh laki 5.
Emanuel Giniki
alifanikiwa kushika nafasi ya tatu na kujinyakulia zawadi ya sh 250,000,nafasi ya nne ikichukuliwa na
Ezekiel Therop huku mwanariadha
Mohamed Msenduki wa klabu ya Wining Spirit ya jijini Arusha akimaliza nafasi ya tano.
Mwanariadha wa kike Failuna aliyerejea hivi
karibuni kutoka nchini Brazil
kushiriki mashindano ya mbio za Km 15 ambazo
alifanikiwa kumaliza mbio hizo
katika nafasi ya saba,aliwaongoza wakongwe kama Banuelia Bryton ,Marry Naali Jackline sakilu na
Catherine Range akimaliza mbio
katika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa 1:10:25.
Failuna aliyejinyakulia zawadi ya kitita cha kiasi
cha sh Mil,1. alifuatiwa kwa
karibu na mpinzani wake Nathalia Elisante aliyetumia muda wa 1:14:40 na kuzawadiwa kitita cha sh
500,000 huku nafasi ya tatu
ikichukuliwa na Magdalena Crispine aliyetumia muda wa
1:15:56, nafasi ya nne na
tano ikienda kwa Anjelina Tsere na Merry Naali.
Mbio za kimataifa Ngorongoro Marathoni zinafanyika
zikiwa na lengo la kuwawezesha watoto
wa jamii ya kimasai kupata elimu ikiwemo kumalizia shule ya Endulen iliyoko Ngorongoro na kutangaza
urithi wa utalii kupitia hifadhi ya
taifa ya Ngorongoro huku ikishirikisha pia mbio za Kilomita tano kwa wafanyakazi wa taasisi
mbalimbali pamoja na Km 2.5 kwa wanafunzi.
Kwa picha zaidi ingia hapa,
www.dixonbusagaga.blogspot.com
|
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment