GIDAMIS SHAHANGA ni mwanariadha maarufu sana wa miaka ya
70 naa... hadi
1990
aliyeliletea Taifa letu la Tanzania heshima na rekodi isiyofutika
katika rekodi sahihi za riadha nchini Tanzania na kote duniani.
Gidamis ndiye mwanariadha wa kwanza hadi sasa ambaye picha yake iliwekwa katika
STAMP (ya barua) ya Tanzania mnamo mwaka
1980 wakati wa utawala wa Mhasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Gidamis Shahanga ni mwanariadha mstaafu aliyekuwa amejikita katika mbio
ndefu za mita 10,000 na mbio za Marathon. Shahanga alizaliwa Septemba
4, 1957 kaskazini mwa Tanzania yani Katesh Wilayani Hanang Manyara.
Kutoka kushoto (25) ni Zacharia Barie (Mtanzania) na katikati (26) ni
GIDAMIS SHAHANGA wakimuonyesha umahiri mkenya (23) katika mbio
zilizofanyika San Juan Porto Rico miaka ya 1980.
Ni vyema serikali na wadau wa michezo nchini kuwaenzi wachezaji wa
zamani walioliletea Taifa letu heshima katika michezo mbali mbali hapa
nchini kama
Gidamis Shahanga. Kwa pamoja Site hii ya
Asili Yetu Tanzania inampongeza sana bwana
Gidamis Shahanga kwa kuonyesha ushujaa wake katika mchezo wa riadha hapa nchini miaka ya 70.
HAYA NI BAADHI YA MAFANIKIO YAKE YA KIMATAIFA
Source: Victormachota.
0 Comments