Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB)
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin
alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB)
akielezea jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution
ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini
Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin na kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB)
akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin
alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB)
akifurahia jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution
ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini
Dar es Salaam. Kutoka kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi
Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin, Mkurugenzi wa Masuala ya
Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa na Mkurugenzi Mkuu wa Excutive
Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB)
akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin
(kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano
wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi.
Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia).
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB)
akikabidhiwa zawadi kutoka TBL kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL
Group Roberto Jarrin (kushoto) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Lager
alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka
kulia) na Meneja Masuala ya Nje na Mawasiliano Bibi. Emma Oriyo.
Picha Zote na: Frank Shija, WHUSM.
Na: Frank Shija, WHUSM
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni
yatakayofanyika tarehe 28 Februari kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi.
Hayo
yamebainisha na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution ambayo
ndio waratibu wa mbio hizo Bw. Aggrey Marealle walipotembelea ofisini
kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.
“Mbio
za Kili Marathon zinatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika
viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ambapo mgeni rasmi atakuwa
Mhe. Nape Moses Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo”.
Alisema Marealle.
Marealle
alisema kuwa Mbio hizo zitakuwa katika makundi manne ambayo ni mbio za
Kilomita 42 ambazo ndiyo marathoni yenyewe inayothaminiwa na TBL kupitia
bia ya Kilimanjaro,zingine ni Nusu Marathon za kilomita 21
zinazodhaminiwa na Tigo,mbio za kilomita 10 zinazowashirikisha walemavu
wanaotumia Baiskeli za matairi matatu na Viti vya matairi
zinazodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Gapco na mbio zinginge ni za
kilomita 5 ambazo zinadhaminiwa na TBL kupitia kinywajji cha Grand Malt
Aliongeza
katika mbio hizo washindi kumi kila kundi watapewa zawadi ambapo
mshindi wa kwanza kwa mwanaume na mwanamke katika mbio za kilomita 42
watapatiwa zawadi ya shilingi milioni nne kila mmoja.
Aidha
alisema kuwa zaidi ya washiriki 7000 wanakadiriwa kushiriki mbio hizo
huku kati yao takribani washiriki 1000 watatoka nje ya nchi.
Kilimanjaro
Marathon inatimiza miaka 14 tokea kuanzishwa kwake ambapo waandaji wa
mashindano hayo ni Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini na
kuratibiwa na Executive Solutions Ltd ya Tanzania na mdhamini mkuu wa
mbio hizo ni Kampuni ya Bia TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro Lager.
0 Comments