Profesa Elisante Ole Gabriel |
Chama Cha Riadha Tanzania (RT) kilifanikiwa kujadili na
kupitisha katiba yake mjini Morogoro.
Mkutano huo mkuu uliohudhuriwa na wajumbe wa mikoa 18 na
kamati ya utendaji wa chama hicho ulifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel.
Pamoja na vifungu vyote vilivyokuwa katika ‘Draft Proposal’
kupita lakini muhimu zaidi ni kipengele kilchoweka ushiriki maalum wa Zanzibar
katika chama hicho.
Mkutano ulifanyika na kumalizika salama chini ya uenyekiti
wa rais wa shirikisho hilo Anthon Mtaka (DC Hai) na Katibu wake Suleman Nyambui
huku maelezo ya kisheria yakifafanuliwa na mwanasheria wa RT Thabit Bashir.
0 Comments