Na Mwandishi Wetu
RIADHA
Tanzania (RT) kwa kushirikiana na Benki ya Azani, leo wametangaza
zawadi kwa washindi wa mbio za watoto, Kids Run, zitakazofanyika
Juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya RT, Tullo Chambo alisema mbio hizo zitakuwa katika vipengele vitano
vya umbali wa kilometa tano, mbili na moja, huku zingine ni meta 100 na meta 50
kwa wavulana na wasichana kulingana na umri.
Alisema wale wa kilometa tano, mbili na moja wenyewe watapita
katika barabara mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kumalizia mbio hizo
katika viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja walikoanzia.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Kids Run zitakazofanyika Mei 5 jijini Dar es Salaam. |
Alisema maandalizi yanaenda vizuri na ni matarajio yao kuwa zaidi
ya watoto 2,000 watajitokeza kushiriki katika mbio hizo za kwanza na aina yake
kushirikisha watoto.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa benki ya Azani, Othman Jibrea alisema
kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa tano ataondoka na sh. 200,000, suti
ya michezo na vifaa vya shule.
Mratibu wa Kids Run, Wilhelm Gidabuday akizungumza leo kuhusu mbio hizo. Kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya Azania, Othman Jibrea. |
Mshindi wa pili atapewa sh. 150,000 suti ya michezo na vifaa vya elimu,
wakati mshindi watatu atapewa sh. 100,000 na vifaa vya elimu.
Mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa mbili ataondoka n ash.
100,000, wakati wa pili atapewa sh. 75,000 na watatu sh. 50,000, ambapo wote
mbali na zawadi za fedha watapewa vifaa vya shule.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania, RT, Tullo Chambo. |
Jibrea alisema washindi wa kilometa moja watapata zawadi za sh.
75,000, 50,000 na 40,000 pamoja na vifaa vya shule.
Alisema kuwa washindi wote pia watafungiliwa akaunti katika benki
ya Azani, ambako watawekewa zawadi zao hizo.
Aidha,
Benki ya Azani imesema kuwa itatumia zaidi ya Sh.Milioni 130 kugharamia
mashindano hayo, ambayo ni ya kwanza na ya aina yake kufanyika hapa
nchini.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa benki ya Azani, Othman Jibrea akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Kids Run. |
0 Comments