![]() |
| RC Makonda akishuhudia makubaliano |
BENKI ya Azania imeingia makubaliano na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kuendesha mashindano ya riadha kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 yajulikanayo kama Kids Run Dar es Salaam yatakayofanyika Juni 5.
Hafla ya makubaliano hayo ilifanyika jana na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Benki hiyo imewekeza shilingi milioni 130 kwa ajili ya mbio hizo. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania, Godfrey Dimoso, alisema benki hiyo inamilikiwa na Watanzania na wamejitosa kudhamini mbio hizo baada ya kukubaliana na RT.
“Hili kwetu ni tukio la kihistoria kwa kuwa benki yetu ni ya kwanza kudhamini riadha tukiwa sekta binafsi, hivyo tumekubaliana na wenzetu wa RT kushirikiana katika hilo,” alisema Dimoso. Kwa upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa RT, William Kalaghe, alisema ni mara ya kwanza mashindano hayo kupata wadhamini nje ya Serikali, hivyo itasaidia katika kukuza vipaji vya watoto.
“Hili ni tukio la kihistoria kwetu RT kupata mdhamini nje ya Serikali, tunatarajia watoto zaidi ya 2,000 watashiriki mbio hizi. “Miji mingi duniani imekuwa maarufu kutokana na riadha, nasi tunaamini kuwa mbio hizi zikisimamiwa ipasavyo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza mji wetu wa Dar es Salaam,” alisema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda, aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema watoto wengi wana vipaji, lakini hawapati fursa ya kuendelezwa.
“Kama hatujawekeza kwa watoto, hatuwezi kuendelea kama taifa, michezo si burudani pekee, bali pia ni uchumi wa mataifa mbalimbali, sisi tunazidi kushuka kwa kuwa hatuoni faida ya michezo, lakini tukijipanga vema tutaondokana na uhalifu, vijana watalitangaza taifa na pia kupunguza tatizo la ajira,” alisema Makonda.
Chanzo: Mtanzania





Kocha wa timu ya taifa ya riadha Fracis John (kulia) akiwa na
wanariadha wanaounda timu ya taifa ya riadha wakitizama msaada wa Track
Suit ulitolewa na GSM Foundation kwa ajili ya wanariadha hao.
Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akitizama
msaada wa track suit zilizotolewa na kampuni ya GSM Foundation.
Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akikabidhi msaada wa track Suit zilizotolewa na GSM Foundation .
Wanariadha wanaounda timu ya taifa wakichagua Track suit zilizotolewa na kampuni ya GSM Foundation . 
Kila mmoja akichagua rangi anayopendelea.
Wanariadha wanaounda timu ya taifa ,wakiwa katika picha ya pamoja na
rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka pamoja na kocha
wao Francis John .











Walemavu
wakianza kutimua mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016
zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini
Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mmoja
ya walemavu Vosta Peter (30) kutokea Dar es Salam akiongoza katika mbio
za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa
na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki
iliyopita.







