The Kit for Alphonce Felix Simbu, Ready for the Race, World Athletics Championships Tokyo 2025 Japan, Sponsored by Xtep Gears
The Kit for Alphonce Felix Simbu, Ready for the Race, World Athletics Championships Tokyo 2025 Japan, Sponsored by Xtep Gears
Wanariadha wa Kimataifa , Alphonce Felix Simbu na Josephat Joshua Gisemo kuipeperusha Bendera ya Tanzania leo Usiku kwenye Mashindano ya Dunia (World Championships 2025) ya Riadha huko Tokyo Japan.
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) limepanga kuweka sheria mpya itakayowalazimisha wandaaji wa mashindano kuhakikisha wanajumuisha pia mbio za watoto katika kila tukio litakaloandaliwa.
Hatua hiyo inalenga kujenga msingi imara wa vipaji na kuwekeza mapema kwenye maendeleo ya riadha nchini.
Rais mpya wa RT, Rogath John Stephen Akhwari, alisema mpango huo utahusisha kuandaa mashindano maalumu ya watoto na vijana kwa kila kanda, yakiratibiwa kwa kushirikiana na vyama vya mikoa ili kuhakikisha kunakuwepo mtiririko wa mashindano kuanzia ngazi ya chini.
Akhwari alibainisha kuwa wapo mbioni kuandaa kanuni mpya za kusimamia mbio za barabarani, ambapo kutakuwa na utaratibu wa kutofautisha mashindano ya kimaifa yatakayosimamiwa na RT moja kwa moja na yale ya ndani yenye malengo ya kitaifa, kwa lengo la kuongeza ubora na hadhi ya riadha nchini.
“Hizi mbio itakuwa ni lazima, siyo chaguo tunataka kuboresha kanuni zetu na yeyote atakayehitaji kibali cha kuandaa mashindano atalazimika kuhakikisha mbio za watoto pia zitakuwepo,” alisema Akhwari.
Alieleza watapeleka wataalamu waliobobea ili kusaidia wandaaji kuelewa namna sahii ya kuandaa mashindano ya watoto, akisisitiza kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo awali ni watoto kukimbia mbio ndefu zisizolingana na umri wao.
"Watoto wetu wamekuwa wakikosa fursa hizi, kwa sababu mara nyingi wakipewa mbio wanakimbizwa umbali wa kilometa tano, hapo awali tulivumilia kwa sababu tulikuwa hatuna mfumo madhubuti lakini sasa tunataka kubadilisha hilo,” aliongeza.
Aidha kabla ya sheria mpya kupitishwa, RT imesema itatoa elimu kwa wandaaji wote wa mbio, kisha kuwapa muda wa maandalizi kabla ya utekelezaji rasmi.
Akhwari anasema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha riadha Tanzania inakua kwa kuanzia watoto, vijana hadi kuzalisha wanariadha wa kiwango cha kimataifa.
Imeandaliwa na Mwananchi Communications Limited
Kocha Mwingereza akimpongeza rais wa shirkisho la Riadha Tanzania -RT Kocha Rogath John Stephen Akhwari wakati wa mapokezi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Leo.
Na John Mhala, Arusha.
ARUSHA: Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Rogath John Stephen Akhwari amesema safari ya kuendeleza mchezo wa riadha ndio imeanza kwani shirikisho hilo litaanzisha rasmi mbio za watoto na vijana lengo ni kuwatayarisha wenye umri huo kuwa kurithi mikoba ya wanariadha wanaojiandaa kustaafu.
Stephen amesema hayo leo alfajiri alipowasili jijini Arusha akitokea Mwanza baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa RT kuwa Rais wa Shirikisho hilo na kusema kuwa wakati umefika sasa wa kuwaandaa watoto na vijana kushiriki mchezo wa riadha ili waweze kushika nafasi za akina Alphonce Simbu ,Magdalena Shauri,Jackline Sakilu na Gabriel Geay watakapostaafu.
Amesema RT lazima ijiandae kwa kuwaanda watoto na vijana ili waupende mchezo huo na hatimaye waweze kufanya vizuri kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na kushika zile nafasi walizofanya vizuri wanariadha wenzao hivyo wale wote wanaoanzisha na walioanzisha mbio kote nchini kipaumbele ni kuanzisha mbio za watoto na vijana mara moja kwani ndio lengo la msingi la kukuza mchezo huo unapendwa kwa sasa hapa nchini.
Rais huyo amesema ajira kwa sasa ni ngumu iwe ndani ya serikali na nje ya serikali na ajira nzuri ni mchezo wa riadha hivyo aliwaasa wazazi kuwapa ushirikiano watoto na vijana kujikita katika mchezo huo kwani una pesa nyingi kwa muda mfupi na kutoa mfano Simbu aliposhinda mbio za Boston amepata fedha nyingi ambazo hata waziri akistaafu serikali hawezi kuzipata.
Rogath ambaye mwajiriwa wa jeshi la Polisi nchini na kituo chake cha kazi Polisi Kati Arusha kwa cheo cha Mrakibu Msaidizi Mwandamizi (ASP) alimshukuru sana Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Inspekta General wa Polisi, Camilius Wambura kwa kumpa baraka za kuchukua fomu za kuwania kinyang’anyanyiro hicho na hatimaye kushinda urais.
Kocha wa Polisi Tanzania na Katibu Mkuu wa Riadha Chama cha Mkoa wa Arusha Rogath John Stephen Akhwari amechaguliwa na wajumbe kuwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania huko Mwanza tarehe 16/08/2025 kwa kupata Kura 27 kati ya 47 na mpinzani wake Bw. Nsolo Malongo Mlozi kupata kura 20.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya benki ya NBC akiwa sambamba na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw Theobald Sabi, Dkt Ndumbaro pamoja na kusifia jitihada za benki hiyo katika kuinua sekta ya michezo nchini, alisema kwasasa taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa wanariadha wenye sifa ya kushiriki mashindano ya kimataifa hivyo serikali imejipanga kutumia mbio hizo kutambua wanariadha wenye sifa sahihi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano mbalimbali ya kimataifa.
“Kwasasa kwenye mashindano ya Olympic tunakwenda na wanariadha wachache sana kwasababu hatuna maandalizi ya kutosha. Hivyo NBC Dodoma Marathon ni moja ya chanzo cha kupata wanariadha wazuri ili baada ya mbio hizi tuweze kuwatamuba na kuwapa mafunzo zaidi ili mashindano ya ‘Commonwealth’ na Olympic na mengine mbalimbali ya kimataifa tuwe na wanariadha wengi zaidi.’’ Alibainisha Dkt. Ndumbaro huku akipongeza maandalizi ya mbio yenye kuzingatia viwango vya kimataifa.
Aidha Dkt. Ndumbaro aliipongeza benki hiyo kwa jitihada mbalimbali za kuendeleza sekta ya utamaduni, sana ana michezo kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo udhamini wa michezo na huduma za kibenki zinazolenga kuwasaidia wadau mbalimbali wa sekta hizo.
“Tofauti na mbio hizi, jitihada za benki ya NBC kwenye kuinua sekta ya michezo zinaonekana kupitia udhamini wake kwenye ligi za NBC Premier League, NBC Championship na NBC Youth league ambapo imewekeza kiasi cha Sh.32.6 Bilioni kwenye ligi hizo. Pia benki hii ina inashiriki katika uwezeshaji kiuchumi kwa wasanii kupitia mfuko wa maendeleo ya sanaa nchini sambamba na kusimamia kamati ya Hamasa ya Timu za Taifa ambapo mpaka sasa imeshakusanya kiasi cha Shilingi 2 bilioni kati kutokana na ahadi za awali za Sh.4 bilioni zilizopokelewa katika hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo,’’ alisema.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Sabi alisema jitihada za benki hiyo katika kuendeleza sekta ya michezo nchini kwa kiasi kikubwa inachagizwa na imani ya benki hiyo kuwa sanaa na michezo ni nguzo ya ajira na kuunganisha taifa.
“Kwa mfano kupitia udhamini wetu kwenye ligi tatu muhimu za mpira wa miguu hapa nchini, mbali na kuzalisha vipaji tumezalisha ajira za moja kwa moja zaidi ya 7,000 na mamilioni ya ajira zingine kwenye mnyororo wa uchumi. Zaidi pia kupitia mbio hizi za NBC Dodoma Marathon kwa kushirikiana na wadau wetu mbalimbali tunalenga kukusanya fedha kusaidia juhudi za Serikali katika kuboresha ya afya ya mama na mtoto kupitia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kutoa ufadhili kwa wakunga,’’ alisema.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) akipokea sweta maalum la mbio za NBC Dodoma Marathon kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi ikiwa ni ishara ya kumkaribisha rasmi Waziri huyo kwenye mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma zikiwa na lengo la kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto Makabiziano hayo yamefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) akimpongeza Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) baada ya kuthibitisha dahamira yake ya kukimbia km 42 kwenye mbio za NBC Dodoma Marathon zinazoratibiwa na benki hiyo kwa lengo la kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto. Dkt Ndumbaro amethibitisha dhamira hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) akimpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon Bi Tatiana Masimba kwa maandalizi mazuri yam bio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma zikiwa na lengo la kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mbio za NBC Dodoma Marathon pamoja mchango wa benki ya NBC katika kuendeleza sekta ya michezo nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mbio za NBC Dodoma Marathon pamoja mchango wa benki ya NBC katika kuendeleza sekta ya michezo nchini. Kushoto ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro.
Wanariadha 8 wakiwemo wa Mbio za Uwanjani, Mbio ndefu na Mrusha mkuki, wameondoka kwenda Accra , Ghana kushiriki mashindano ya Afrika “All African Games” ambayo yalianza toka tarehe 8 Machi hadi 23 Machi 2024.
Copyright @gettyimages
Hongera kwa Andrew Boniface Rhobi kutoka jeshi la polisi Tanzania kwa kupata muda wako bora wa dakika tatu na sekunde hamsini na moja ( 3:51.44) yaani ( Personal Best) mita 1500 (1500M) na kuwa nafasi ya Saba kwenye heat ya kwanza, kwenye Mashindano ya Dunia ya Ndani ( World Athletics indoors Championships Glasgow 2024) tarehe 1-3 Machi 2024, huko Glasgow, Scotland.
BINGWA wa Taifa anayeshikilia rekodi ya Marathon Tanzania, Gabriel Gerald Geay amekuwa kivutio kikubwa Mbeya Tulia Marathon, aliposhiriki na kuibuka mshindi katika mbio za mita 1500.
Mbeya Tulia Marathon, imekata utepe Leo Mei 5 kwa mbio za uwanjani, kabla ya kesho Jumamosi Mei 6 kurindima Marathon.
Katika mbio hizo za mita 1500, Geay alianza taratibu raundi ya kwanza akiwa nyuma, kabla ya mzunguko wa pili kupata dhoruba la kuangushwa, lakini alinyanyuka na kukiwasha na hatimaye kuibuka mshindi akitumia dakika 3:58.46.
Geay alifuatiwa na Faraja Damas wa JWTZ aliyetumia dakika 4:00.08 huku nafasi ya tatu ikienda kwa John Joseph pia JWTZ 4:06.25.
Mashabiki na viongozi mbalimbali waliojitokeza, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa, walishindwa kujizua kumshangilia Geay wakati akikiwasha katika mbio hizo.
Kwa upande wa wanawake Mita 1500, Magdalena Shauri wa JWTZ, alishinda akitumia dakika 4:31.13 na kufuatiwa na Salma Charles ambaye katoka Zambia na Timu ya Taifa U 18 na 20 iliyoshiriki mashindano ya Afrika, dakika 4:46.55 na wa tatu akiwa ni Mayselina Mbua JWTZ 4:53.16.
Mbali na Geay ambaye katoka kufanya kweli katika mbio kongwe za Boston Marathon nchini Marekani alikoshika nafasi ya pili hivi karibuni, pia mkali mwingine, ambaye pia ni Mshindi wa medali ya Fedha Jumuiya na Mwanamichezo Bora Tuzo za BMT 2022, Alphonce Simbu, naye alikuwepo kushuhudia mbio hizo.
Pia, Timu ya Taifa ya Vijana iliyopumzika hapa ikitokea Ndola Zambia ilikojinyakulia medali mbili katika mashindano ya Afrika, baadhi walipata nafasi ya kushiriki mbio za uwanjani Mbeya Tulia Marathon.
Timu hiyo inatarajiwa kuondoka Mbeya kesho Jumapili kurejea Dar es Salaam.
Pia, mbio hizo zilipambwa program ya watoto 'Kids Athletics', ambayo ilikuwa kivutio kwa watoto wa shule za msingi walioshiriki.
NA TULLO CHAMBO, RT
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), kwa ushirikiano na shirikisho la mchezo huo nchini Kenya (AK), wamezindua kifaa maalum cha kupima hali ya hewa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kifaa hicho ni maalumu kwa ajili ya kupima ubora wa hali ya hewa sehemu husika, kama iko sawa kwa matumizi ya wanamichezo shiriki wakati wa tukio ama haiko sawa.
Ufungaji wa kifaa hicho ni maagizo ya Shirikisho la Riadha la Kimataifa (WA), ambapo Tanzania imekuwa nchi ya nne barani Afrika kupata teknolojia hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mbele ya Mgeni rasmi Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha, Rais wa AK ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Riadha Ukanda wa Afrika Mashariki (EAAR), Luteni Jenerali mstaafu Jackson Tuwei, alisema kifaa hicho ni muhimu kwani binadamu hata wanyama wanahitaji kuishi katika mazingira ya hali ya hewa safi.
Luteni Jenelari Tuwei, alisema teknolojia hiyo imeanza kutumika nchini Kenya, kisha ilifuatiwa na Dakar Senegal, Addis Ababa Ethiopia na Tanzania imekuwa ni nchi ya nne kufungwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na badae wanatarajia kufunga kifaa hicho nchini Zambia ambako yanatarajiwa kufanyika mashindano ya vijana Afrika Aprili 27 hadi Mei 3.
Kwa upande wake, Katibu wa BMT, Neema Msitha, alishukuru kwa jambo hilo ambalo linauongezea thamani wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kimataifa, na kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, mbali ya kuipongeza RT kwa kufanikisha jambo hilo lenye manufaa kwa wanamichezo wote watakaokuwa wanautumia uwanja huo, iko tayari kutoa Ushirikiano katika kila jambo lenye maendeleo kwenye sekta ya michezo na kwamba wadau wote wa michezo wanakaribishwa.
Kifaa hicho kimetengenezwa na taasisi ya mazingira nchini Sweden ijulikanayo kama Stocklohom Environment Instute (SEI).
Copyright © 2015 - 2025 Athletics Tanzania All Right Reserved
Developed by Gadiola Emanuel