MCHAKATO
wa usajili wa washiriki wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016,
umezidi kushika kasi, huku siku tatu zikiwa zimesalia kabla ya
kufanyika kwake Juni 5 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Wilhelm
Gidabuday, alisema kufikia jana mchana, mchakato wa usajili ulikuwa
ukiendelea vema, ambako wazazi na walezi wamejitokeza kusajili watoto
wao.
Gidabuday
alisema kuwa, matarajio ni kusajili watoto wapatao 2,000 walio na umri
chini ya miaka 16, ambao watashiriki Azania Bank Kids Run 2016, mbio
zilizogawanywa katika kategori tano za kilomoita 5, km 2, km 1, mita 100
na mita 50.
Alibainisha
kuwa, fomu za ushiriki zinapatikana katika Matawi ya Azania Bank popote
jijini Dar es Salaam, pamoja na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania
(RT), pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.
Aliwataka wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu za ushiriki wa watoto
wao, kuchangamkia mchakato huo kwa kufika katika vituo husika na
kununua fomu hizo kwa shilingi 2,000 tu, ili kuwawezesha watoto
kushiriki na kushinda zawadi.
Naye,
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank inayodhamini mashindano hayo,
Othman Jibrea, alisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kusajili watoto
wao katika Azania Bank Kids Run, ili kufikia lengo lao la kuibua vipaji
vipya vya riadha.
Jibrea
alibainsiha kuwa, Azania Bank imejitosa kudhamini mbio hizo kutokana na
mlengo wake wa kuibua vipaji vichanga katika riadha, hivyo ili kufikia
lengo, wazazui na walezi hawana budi kujitokeza kwa wingi kusajili
watoto wao.
Alizitaja
zawadi za mbio za Kilomita tano kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa
kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa
tatu, wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na
sare za michezo (track suit).
Jibrea
alibainisha kuwa, mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2 atajinyakulia
Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh. 50,000,
pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
Katika
mbio za kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh.
75,000 kwa mshindi wa kwanza, 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000
kwa wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa
vya shule na sare za michezo.
"Pia,
washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh.
15,000, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo. Nia ni kuwafanya
watoto watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano," alisema
Jibrea.














Kocha wa timu ya taifa ya riadha Fracis John (kulia) akiwa na
wanariadha wanaounda timu ya taifa ya riadha wakitizama msaada wa Track
Suit ulitolewa na GSM Foundation kwa ajili ya wanariadha hao.
Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akitizama
msaada wa track suit zilizotolewa na kampuni ya GSM Foundation.
Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akikabidhi msaada wa track Suit zilizotolewa na GSM Foundation .
Wanariadha wanaounda timu ya taifa wakichagua Track suit zilizotolewa na kampuni ya GSM Foundation . 
Kila mmoja akichagua rangi anayopendelea.
Wanariadha wanaounda timu ya taifa ,wakiwa katika picha ya pamoja na
rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka pamoja na kocha
wao Francis John .











Walemavu
wakianza kutimua mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016
zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini
Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mmoja
ya walemavu Vosta Peter (30) kutokea Dar es Salam akiongoza katika mbio
za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa
na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki
iliyopita.





