Matukio mbalimbali ya mashindano ya riadha kwa wanawake " Ladies First 2025 " yanayofanyika katika Uwanja wa Benjamin mkapa. #AthleticsTanzania
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya benki ya NBC akiwa sambamba na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw Theobald Sabi, Dkt Ndumbaro pamoja na kusifia jitihada za benki hiyo katika kuinua sekta ya michezo nchini, alisema kwasasa taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa wanariadha wenye sifa ya kushiriki mashindano ya kimataifa hivyo serikali imejipanga kutumia mbio hizo kutambua wanariadha wenye sifa sahihi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano mbalimbali ya kimataifa.
“Kwasasa kwenye mashindano ya Olympic tunakwenda na wanariadha wachache sana kwasababu hatuna maandalizi ya kutosha. Hivyo NBC Dodoma Marathon ni moja ya chanzo cha kupata wanariadha wazuri ili baada ya mbio hizi tuweze kuwatamuba na kuwapa mafunzo zaidi ili mashindano ya ‘Commonwealth’ na Olympic na mengine mbalimbali ya kimataifa tuwe na wanariadha wengi zaidi.’’ Alibainisha Dkt. Ndumbaro huku akipongeza maandalizi ya mbio yenye kuzingatia viwango vya kimataifa.
Aidha Dkt. Ndumbaro aliipongeza benki hiyo kwa jitihada mbalimbali za kuendeleza sekta ya utamaduni, sana ana michezo kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo udhamini wa michezo na huduma za kibenki zinazolenga kuwasaidia wadau mbalimbali wa sekta hizo.
“Tofauti na mbio hizi, jitihada za benki ya NBC kwenye kuinua sekta ya michezo zinaonekana kupitia udhamini wake kwenye ligi za NBC Premier League, NBC Championship na NBC Youth league ambapo imewekeza kiasi cha Sh.32.6 Bilioni kwenye ligi hizo. Pia benki hii ina inashiriki katika uwezeshaji kiuchumi kwa wasanii kupitia mfuko wa maendeleo ya sanaa nchini sambamba na kusimamia kamati ya Hamasa ya Timu za Taifa ambapo mpaka sasa imeshakusanya kiasi cha Shilingi 2 bilioni kati kutokana na ahadi za awali za Sh.4 bilioni zilizopokelewa katika hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo,’’ alisema.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Sabi alisema jitihada za benki hiyo katika kuendeleza sekta ya michezo nchini kwa kiasi kikubwa inachagizwa na imani ya benki hiyo kuwa sanaa na michezo ni nguzo ya ajira na kuunganisha taifa.
“Kwa mfano kupitia udhamini wetu kwenye ligi tatu muhimu za mpira wa miguu hapa nchini, mbali na kuzalisha vipaji tumezalisha ajira za moja kwa moja zaidi ya 7,000 na mamilioni ya ajira zingine kwenye mnyororo wa uchumi. Zaidi pia kupitia mbio hizi za NBC Dodoma Marathon kwa kushirikiana na wadau wetu mbalimbali tunalenga kukusanya fedha kusaidia juhudi za Serikali katika kuboresha ya afya ya mama na mtoto kupitia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kutoa ufadhili kwa wakunga,’’ alisema.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) akipokea sweta maalum la mbio za NBC Dodoma Marathon kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi ikiwa ni ishara ya kumkaribisha rasmi Waziri huyo kwenye mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma zikiwa na lengo la kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto Makabiziano hayo yamefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) akimpongeza Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) baada ya kuthibitisha dahamira yake ya kukimbia km 42 kwenye mbio za NBC Dodoma Marathon zinazoratibiwa na benki hiyo kwa lengo la kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto. Dkt Ndumbaro amethibitisha dhamira hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) akimpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon Bi Tatiana Masimba kwa maandalizi mazuri yam bio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma zikiwa na lengo la kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama wa mtoto
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mbio za NBC Dodoma Marathon pamoja mchango wa benki ya NBC katika kuendeleza sekta ya michezo nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mbio za NBC Dodoma Marathon pamoja mchango wa benki ya NBC katika kuendeleza sekta ya michezo nchini. Kushoto ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro.
Kutoka Kulia: Ofisa wa BMT Charles Maguzu, Makamu wa Rais William Kallaghe na Mjumbe wa Kanda ya Kaskazini Alfredo Shahanga.
Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania RT , Ndugu William Kallaghe akikabidhi ripoti kwa Katibu Mkuu Mtendaji wa BMT, Bi. Neema Msitha Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu RT, Wakili Jackson Ndaweka.
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limeitaka mikoa yote nchini kuhakikisha inaendesha mashindani ya Vijana chini miaka 20 na 18 'U-20 U-18' kuanzia ngazi ya Wilaya.
Maelekezo hayo yametolewa na Kaimu Katibu Mkuu RT, Wakili Msomi Jackson Ndaweka, katika barua yake ya Januari 25 kwenda kwa viongozi wa vyama vya mikoa Tanzania Bara.
Amewaelekeza viongozi hao, kukumbuka kwamba kuna jukumu kubwa mbele yao, kwani mwaka huu una mashindano mengi ya vijana wa umri huo.
Wakili Ndaweka, aliyataja mashindano hayo kuwa ni Afrika Mashariki U-18 na 20, Tanzania ikiwa mwenyeji, ambapo awali yalikuwa yamepangwa kufanyika Kigali, Rwanda.
Alisema, mashindano hayo yatafuatiwa na ya Afrika kwa umri huo Lusaka, Zambia Aprili 27 hadi Mei 3, 2023.
"Ili kuhakikisha nchi inashiriki kwa mafanikio mashindano hayo, lazima mashindano yaanzie ngazi ya Wilaya, kisha Mkoa na mwisho mashindano ya Taifa ya Wazi kwa vijana wa umri huo ambayo yanatarajiwa kufanyika Februari 25," alisema na kuongeza.
Mashindano ya Wilaya yafanyike kati ya Februari 9-11 na Mikoa Februari 13-19.
"Utaratibu huu, unakusudia kuhakikisha wanapatikana wachezaji wenye uwezo mkubwa, ili kuleta tija katika ushiriki wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa," alisema Wakili Ndaweka.
Sambamba na hilo, RT inakusudia na imejipanga kuhakikisha kuwa kalenda yake inafuatwa na matukio yote yanafanyika kama yalivyopangwa.
Sudan Kusini yaipa shavu RT, Simbu Balozi mpya JICA
NA TULLO CHAMBO, RT
MASHINDANO Maalum ya Riadha ya Wanawake nchini Tanzania maarufu kama Ladies First, yamezidi kufungua ushirikiano wa mchezo huo kimataifa.
Ladies First ikiwa ni wazo la Nguli wa Riadha nchini Tanzania, Kanali mstaafu Juma Ikangaa, imefanyika mwaka huu ukiwa ni msimu wa nne na kushirikisha mikoa 30 Kati ya 31 Tanzania Bara na Visiwani.
Mwaka huu, mashindano hayo yalifanyika January 21 na 22 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kushirikisha zaidi ya wanariadha 186.
Kanali Mstaafu Ikangaa, ambaye enzi zake aliiwakilisha vema Tanzania kimataifa katika mbio za marathoni, ikiwemo nchini Japan, nchi hiyo imekuwa ikimuenzi na kumpa heshima kubwa ambapo hivi sasa ni Balozi wa Hiari wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).
Katika kumuenzi Kanali Ikangaa, Japan ilimtaka kusema kitu ambacho nchi hiyo iifanyie Tanzania, ndipo kwa kushirikiana na wadau wake mbalimbali, akaja na wazo la kuwaenzi na kuhamasisha wanawake kushiriki katika mchezo wa Riadha, hasa ikizingatiwa medali ya kwanza ya kimataifa Tanzania ililetwa na Mwanamke Theresia Dismas mwaka 1964, katika michezo ya All Africa nchini Congo Brazzaville, kupitia mchezo wa Kurusha Mkuki 'Javelin'.
Wazo hilo lilianza kutekelezeka mwaka 2017 kwa mashindano yaliyofanyika Uwanja wa Taifa, sasa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo baadhi ya washindi wamekuwa wakipata nafasi ya kwenda kushiriki mbio za Nagai City nchini Japan.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Tanzania (BMT), Bi. Neema Msitha, aliipongeza JICA na kampuni mbalimbali za Kijapan zinazofanya kazi nchini, Kanali Ikangaa,serikali ya Tanzania na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), kwa kufanikisha mashindano hayo kwa msimu wa nne sasa.
Bi. Msitha, anasema mashindano hayo yalianza mwaka 2017 na kufanyika kwa mafanikio makubwa miaka mitatu mfululizo hadi 2019 kabla kusitishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo janga la UVIKO 19 'Covid 19'.
"Lengo la mashindano haya ni kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike katika michezo hususan Riadha, kutoa fursa kwa wanariadha wa kike kuonyesha vipaji vyao na kuendeleza vipaji vya wanariadha ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano ya kitaifa na kimataifa," anasema Bi. Msitha.
Tangu kuanza kwa mashindano hayo mwaka 2017, Wanariadha wa Tanzania na viongozi wao, wamekuwa wakipata nafasi ya kwenda kushiriki Nagai Marathon, ambapo wanariadha akiwemo Angel John Joseph Yumba, Fabian Nelson Sulle, Fabian Joseph, Alphonce Felix Simbu na wengineo wameweza kung'ara.
Mbali na hilo, Ladies First iliweza kuishirikisha nchi ya Sudan Kusini na kushiriki mashindano ya mwaka 2019 jijini Dar es Salaam.
Mwaka huu 2023, Ladies First imezidi kufungua milango katika mchezo wa Riadha Tanzania, ambapo Sudan Kusini iliwakilishwa na viongozi wake mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo nchini humo, Peter Baptist, Balozi wa nchi hiyo nchini Tanzania, Deng Abel na wengineo.
Baptist katika salamu zake, mbali na kushukuru na kupongeza Tanzania kwa mashindano hayo, anasema na kwao wana mashindano kama hayo yajulikanayo kama 'Umoja na Amani', yakilenga kutumia michezo kuhamasisha amani na umoja katika Taifa hilo ambalo liliandamwa na vita miongoni mwao kwa miaka kadhaa.
Mwakilishi huyo, anasema katika kuendeleza ushirikiano na Tanzania, wanatoa mwaliko kwa wanariadha wanne waliofanya vizuri katika Ladies First 2023 wa mbio tofauti ukiondoa mita 5000 kwenda Sudan Kusini kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika miezi miwili ijayo.
Mbali na fursa hizo zilizojitokeza Ladies First 2023, nyingine ni kwa Mwanariadha anayefanya vema hivi sasa, Mshindi wa Medali ya Fedha Common Wealth Games 2022, Alphonce Simbu, naye kuteuliwa kuwa Balozi wa Hiari JICA, akiungana na Kanali mstaafu Ikangaa.
Haya ni kati ya mafanikio ya Ladies First 2023, na hakika uwajibikaji ukizidi kuongezeka, bila shaka milango zaidi itazidi kufunguka katika medani ya riadha Tanzania.
NA TULLO CHAMBO - AT
NA TULLO CHAMBO
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dr. Dorothy Gwajima, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mashindano Maalum ya Riadha ya Wanawake maarufu kama 'Ladies First' yanayotarajiwa kurindima kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa January 21 na 22 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha, alisema mashindano hayo yamendaliwa na BMT, Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), na kuwezeshwa na Shirika la Maendeleo la Japan ( JICA), na huu ni msimu wake wa nne, yakiwa na lengo la kuwahamasisha wanawake kushiriki katika mchezo wa Riadha.
"Lengo la mashindano haya ni kuwahasisha watoto wa kike kushiriki katika michezo hususan Riadha, kutoa fursa ya wanariadha wa like kuonyesha vipaji vyao na kuendeleza vipaji vya wanariadha ambao watawakilisha nchi katika mashindano ya kitaifa na kimataifa siku zijazo," alisema Msitha.
Alisema mashindano ya mwaka huu, yatashirikisha wanariadha 186 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani yakishirikisha mbio za Mira 100, 200, 400, 800, 1500, 5000, 10000, Kupokezana Vijiti 4x400 na Kurusha Mkuki na kushuhudiwa na watazamaji mbalimbali wakiwemo wanafunzi 1000 kutoka shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya Temeke.
"BMT inaishukuru Sana JICA na kampuni za Kijapan zinazofanya shughuli zake hapa nchini kwa kufadhili mashindano haya kwa mara ya nne, pia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kutoa uwanja ambao utatumika kwa mshindano na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ambayo imetoa ruhusa kwa wanafunzi kushiriki na kujifunza katika mashindano haya," alisema Msitha na kuongeza.
Baraza linaendelea kusisitiza Kamati za Michezo za Mikoa, kuhakikisha zunawezesha ushiriki wa wanaridha wa mikoa yao katika mashindano haya na kuwaomba wananchi wote wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi na Jumapili kushuhudia mashindano hayo ambapo hakuna kiingilio.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, Naofumi Yamura, alisema wanajivunia kuanza kutoa ushirikiano kwa Tanzania toka mwaka 1962 na mashindano ya mwaka huu watayatumia kama maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano wao na Tanzania.
Yamura, alisema mashindano ya mwaka huu yatahudhuriwa na watu mbalimbali maarufu akiwemo Balozi wa Japan Tanzania, viongozi kutoka Sudan ya Kusini, Mwanariadha nguli Kanali mstaafu Juma Ikangaa na mwanariadha anayewika hivi sasa Alphonce Simbu.
Naye Katibu wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Muhidin Masunzu akimwakilisha Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Wakili Jackson Ndaweka, alisema wamejiandaa vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa ufanisi.
Wazo la kuanzishwa mashindano hayo liliasisiwa na Kanali Ikangaa, ambaye pia no Balozi wa Hiari wa JICA, likitokana na kuenzi historia ambapo medali ya kwanza Tanzania kimataifa ililetwa na Mwanamama Thereza Dismas, aliyekuwa akirusha Mkuki.
Copyright © 2015 - 2025 Athletics Tanzania All Right Reserved
Developed by Gadiola Emanuel