PONGEZI/SHUKRANI ZA TOC KWA RAIS MSTAAFU MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUENDELEZA MICHEZO KATIKA MIAKA 10 YA UONGOZI WAKE

December 31, 2015
TOC

Napenda kuchukua nafasi hii kuushukuru uongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa kuandaa hafla ya kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 bora waliofanya vizuri kwa kuiletea heshima  nchi yetu katika miaka 10 ya uongozi wa mwanamichezo mwenzetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na kutoa tuzo kwa Wanamichezo bora waliofanya vizuri miaka 10 iliyopita,  vile vile TASWA ilimtunuku tuzo Mhe Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wako katika michezo.

Mhe. Rais, wakati anazungumza na wanamichezo waliokusanyika katika ukumbi wa Mlimani hapo tarehe 12/10/2015 alisononeka kwa wanamichezo wa Tanzania kutofanya vizuri wakati wa miaka 10 ya uongozi wake pamoja na kuleta walimu katika baadhi ya vyama vya michezo.

Mafanikio hata katika maisha ya kawaida ni mapambano hali kadhalika hata kupata mafanikio katika michezo ni mapambano. Katika miaka ya 70-80 michezo ilikuwa ridhaa, lakini kuanzia miaka ya 90 hadi sasa michezo imekuwa biashara na ajira kubwa kwa wanamichezo.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa akimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuendeleza michezo katika kipindi chake chote cha uongozi wake wa miaka 10.
Kwa mfumo huo wa michezo kuwa biashara na ajira kila moja angefikiria kwamba tungepaswa kuwa na wanamichezo wengi  kwa hiari yao kuchangamkia mazoezi ya hali ya juu ili nao waweze kuwa wawakilishi wazuri wa nchi yetu na kujipatia zawadi nono za fedha, lakini badala yake hali inazidi kuwa mbaya.

Hali hii inawezekana vile vile imesababishwa na hali ya ukata wa vyama vya michezo ambao hawana uwezo wa kutafuta vipaji huko walipo hasa Vijijini, Wilayani na Mikoani.

Katika miaka ya 70-80,  Vyama vyetu vilikuwa vinapata ruzuku kutoka Serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ruzuku ambayo ilikuwa inawasaidia kuendesha ofisi na kuandaa Mashindano  kama ya Taifa ambayo wanamichezo wengi wanakusanyika na vyama husika kufanya uteuzi wa wachezaji bora wenye vipaji ambao huwaendeleza.
Huo mfumo kwa sasa haupo kutokana na hali inayotamkwa na vyama vya michezo kama ukata na Serikali (BMT) kutokuwa na fedha.

Katika risala yake wakati wa tuzo kwa wanamichezo bora, Mhe. Rais alikiri bila kuwekeza tusitegemee kupata mafanikio, lakini nani awekeze, kwa haraka kwa tulio na uelewa mdogo ni Serikali ndiyo iwekeze kama nchi zingine duniani inavyofanya.

Mhe. Rais amefanya mengi kuinua michezo wakati wa uongozi wake. Naomba nitaje chache:
1.     WALIMU WA MICHEZO KUTOKA NJE.
Aliweza kuwalipa mishahara walimu wa michezo kama mpira wa miguu, netiboli, ngumi na riadha (pamoja na walimu wa riadha kutokuwa wa viwango) kupitia mpango wa ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba. Kila mmoja wetu aliona jitihada zake,  na nakiri kwamba kwa namna moja au nyingine, vyama/mashirikisho ya michezo hawakutekeleza wajibu wao kutokana na hali ya ukata.

Hata wanamichezo wetu hawakutambua na kuona michezo kama ajira.
Mhe. Rais anakiri mafanikio yana gharama, bila nchi kuwekeza hafikirii kama tutakuwa na mwelekeo mwema hasa kwa vijana wetu kufanya vizuri katika medani ya Kimataifa. Nchi nyingi zinazofanya vizuri katika michezo ya kimataifa  kwa asilimia kubwa wamewekeza katika michezo. Pamoja na WHVUM kutengewa bajeti ndogo ya michezo, bado suala la kuwekeza haliwezi kukwepeka kwa hali ya sasa ya michezo duniani.

2.    MICHEZO YA UMITASHUMTA/UMISSETA.
Tutakukumbuka hasa pale Mhe Jakaya aliporejesha michezo ya Umitashumta na Umisseta  mwaka 2007 baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka 9.
 
Binafsi naamini kilichotufikisha hapa tulipo leo ni pamoja na kutofundishwa kwa elimu ya viungo (PE) sambamba na kutokuwepo walimu wa masomo hayo kwenye shule zetu na kusimama kwa michezo hiyo  na  Michezo ya Majeshi (BAMATA).

Michezo ya Umitashumta/Umisseta ndiyo ilikuwa kiwanda cha kuandaa wachezaji ambapo wanapofanya vizuri hupata ajira katika taasisi za Serikali (JWTZ, Polisi, Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa) lakini kwa sasa imekuwa tofauti kwani taasisi hizo haziajiri kama ilivyo huko nyuma kutokana na kutofanyika Michezo ya Majeshi (BAMATA) ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.

Ni zaidi ya miaka 8 tangu aliporejesha michezo ya Umitashumta/Umisseta kwa nia na madhumuni ya kupata vipaji vitakavyoendelezwa na kuwa na nafasi nzuri ya kutuwakilisha Kimataifa.

Imekuwa vigumu kuendeleza  vipaji vinavyoonekana katika michezo hiyo kwani hakuna maandalizi yaliyofanywa kuwaendeleza  baada ya michezo hiyo kumalizika. Hata wale wanaomaliza masomo yao katika ngazi husika hawapati ajira kutokana na taasisi za Serikali nilizotaja kutokuwa na ajira rasmi kama ilivyo zamani. Mpaka sasa ni shule chache za binafsi  na taasisi zimekuwa na  mpango wa kuwasajili katika shule zao wanafunzi wazuri wenye vipaji na baadhi yao kutoa elimu bure (Scholarships) na kuwaendeleza katika baadhi ya michezo:

a.Shule ya Sekondari ya Alliance, Mwanza (Mpira wa Miguu na Riadha).

b.Shule za Filbert Bayi, Mkuza, Kibaha Mkoa wa Pwani (Riadha na Netiboli)


c.Shule ya Sekondari ya Lord Baden Powel, Bagamoyo (Mpira wa Miguu kwa Wanaume na  Wanawake,  Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu na Riadha).

d.Shule ya Sekondari ya Winning Spirit, Arusha (Riadha)

e.Shule ya Sekondari ya Makongo, Dar Es Salaam (Mpira wa Miguu, Netiboli Kikapu na Wavu).

Naomba niishauri Serikali (Wizara ya Elimu na Tamisemi) kuunda Kanda ili kila baada ya michezo ya Umitashumta na Umisseta wanamichezo wenye vipaji wawekwe katika shule zilizo katika Kanda zitakazoundwa wakiendelea na masomo hali kadhalika na kucheza kwa Wizara husika kupeleka wataalamu (coaches) katika Kanda husika. Kama hilo haliwezekani, basi shule binafsi na taasisi zisaidiwe ili ziweze kuimarisha zaidi mipango waliyonayo ya kuendeleza michezo

Bila kuwa na utaratibu na mipango mahsusi, michezo ya Umitashumta na Umisseta,  itakuwa kama tamasha tu.

3.     UWANJA WA TAIFA
Hakuna ubishi kwa ushiriki wake katika ujenzi wa uwanja wa Taifa wakati wa uongozi wa Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa kama Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mpaka alipochaguliwa kuwa Rais wa awamu ya nne na kumalizia kazi za ujenzi zilizobaki.

Uwanja wetu ni mzuri sana, lakini matumizi yake kwa mchezo wa riadha yamekuwa nadra sana kutokana na gharama kubwa ambayo wakati mwingine  Riadha Tanzania inashindwa kuchangia hasa inapotaka kufanya michezo ya Taifa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.

4.     MAFANIKIO YA MICHEZO WAKATI WA UONGOZI WAKO.
Mhe. Jakaya wakati wa uongozi wake wa miaka 10 kulikuwa na mafanikio ambayo hayaridhishi kwa nchi kama Tanzania yenye watu zaidi ya Milion 45, lakini kutokana na hali halisi niliyotaja hapo juu naomba nitaje mafanikio hayo kama ifuatavyo:

Samson Ramadhani
1.Samson Ramadhani NYONYI, (Riadha):”Marathon”>Dhahabu: Michezo ya Jumuiya ya Madola, Melbourne, Australia 2006.

2.Fabian Joseph NAASI, (Riadha): Mita 10000>Shaba: Michezo ya Jumuiya ya Modola, Melbourne, Australia 2006.
Fabian Joseph.
3.Martin SULLE, (Riadha) Km 21.1>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Algiers, Algeria, 2007.

4.Timu ya Netiboli, (Netiboli)>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Maputo, Msumbiji, 2011.

5.Timu ya Netiboli (Netiboli)>Kushinda Kombe la Mataifa 6, Singapore, 2012.

6.Timu ya Netiboli (Netiboli>Nafasi ya Pili, Mashindano ya Africa, Dar Es Salaam, 2012.

7.Timu ya Mpira wa Miguu watoto wa Mitaani (Street Children World Cup)>Dhahabu, Mashindano Kombe la Dunia, Rio de Jeneiro, Brazil, 2014.

8.Timu ya Mpira wa Miguu-Vijana chini ya Miaka 15>Medali ya Fedha> Michezo ya Vijana Afrika, Gaborone, Botswana, 2014.

5.     SHUGHULI ZA TOC.
Wakati wa uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Olimpiki Tanzania imeweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa vyama vya michezo, baadhi ya hizo shughuli zilikuwa ni kuendesha mafunzo ya ufundi kwa walimu wa michezo kutoka Vyama/Mashirikisho ya michezo wanachama wa TOC kwa kuleta Wakufunzi kutoka nje ya nchi hali kadhalika na Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kwa viongozi wa Vyama/Mashirikisho ya Mikoa na Taifa kwa nyakati tofauti.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi (kushoto) akizungumza kabla ya kuwakabidhi hati wachezaji watatu wa Tanzania waliodhaminiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kupiga kambi Eldoret nchini Kenya. kutoka kulia ni Fabian Joseph, Fabian Nelson na Bazil John.
Kwa ujumla Walimu 523 (448/75) na viongozi 380 (304/76) waliweza kupata elimu ya kufundisha wachezaji kwa madaraja tofauti na uongozi na utawala bora.
(Orodha Nyongeza “A” na “B”imeambatanishwa).

HITIMISHO
Kwa niaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania na kwa niaba yangu napenda nichukue nafasi hii kumshukuru Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kutoa posho za kujikimu, mavazi ya taifa, vifaa vya mazoezi na mashindano timu zetu za Taifa zilizowahi kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola (Melbourne, Australia 2006, New Delhi, India 2010 na Glasgow, Scotland 2014) na Olimpiki (Beijing, China 2008, London, Uingereza 2012).
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akisaini moja ya hati za kuwadhamini wanariadha watatu wa Tanzania kupiga kambi Eldoret, Kenya huku Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania, Suleuman Nyambui akishuhudia. Kushoto ni Rais wa TOC, Gulam Rashid.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru Mhe. Bernard Camillius Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ushirikiano na WHVUM kuwatafutia mazoezi ya nje (China, Ethiopia, Uturuki na New Zealand) kwa kutumia mpango wa Diplomasia ya Michezo (Sports Diplomacy) wanamichezo wetu kabla ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, yaliyofanyika Glasgow, Scotland mwaka jana (2014).

Akiwa kama mwanamichezo nambari moja hata baada ya kustaafu bado wanamichezo wenzako tutahitaji ushauri wake katika maendeleo ya michezo katika
nchi yetu.

Mwisho kabisa natoa wito kwa wanamichezo wote kujitokeza na kutumia haki yao ya Kikatiba hapo Jumapili tarehe 25/10/2015 kupiga kura kuchagua mafiga matatu (Diwani, Mbunge na Rais) kwa kipindi cha miaka 5 (2015-2020) ijayo.

Nawatakia Wanamichezo wote kila la kheri katika mchakato mzima na tulinde  amani tuliyonayo.

Filbert Bayi,


KATIBU MKUU.

Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Mwaka wa TOC unaofanyika Kituo cha Amani, Welezo Zanzibar

December 31, 2015
TOC
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akisoma taarifa yake ya mwaka katika Mkutano Mkuu wa TOC Kituo cha Amani Welezo, Zanzibar. Kulia ni Rais wa TOC Gulam Rashid na Mhazini msaidizi Juma Zaidi (kushoto).
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wakati wa mkutano huo jana Zanzibar.
 







Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid wakati wa ufunguzi  wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa mwaka wa TOC unaofanyika leo Zanzibar. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi na Mhazini Mkuu Charles Nyange.




Mhazini Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Charles Nyange (kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya mmoja ya makampuni yaliyodhamini Siku ya Olimpiki.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TOC katika picha ya pamoja mjini Zanzibar.
 

RISALA YA KATIBU MKUU (TOC) KWENYE UFUNGUZI WA KAMISHENI YA WANAMICHEZO ZANZIBAR TAREHE 10/12/2015.

December 31, 2015
TOC




Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kamisheni ya Wachezaji ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (Kawata) leo Zanzibar. Kushoto ni mwenyekiti wa Kawata, Ramadhan Zimbwe. Kushoto kwa Bayi ni Katibu Msaidizi wa TOC Jamal Adi na rais wa Toc Gulam Rashid.

 TANZANIA OLYMPIC COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA

RISALA YA KATIBU MKUU (TOC), FILBERT BAYI KWENYE UFUNGUZI WA KAMISHENI YA WANAMICHEZO ZANZIBAR TAREHE 10/12/2015.

Ndugu Mgeni Rasmi Jamal Adi, Katibu Mkuu Msaidizi TOC

Ndugu Gulam Rashid, Rais wa TOC,

Ndugu Ramadhani Zimbwe, Mwenyekiti, KAWATA Taifa,

Ndugu Amina Ahmed, Katibu KAWATA Taifa

Viongozi Kamati yaUtendaji Waalikwa

Kamati ya Utendaji, KAWATA Taifa,

Wanamichezo Washiriki

Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe sina budi kumshukuru Katibu Mkuu Msaidizi wa TOC, pamoja na kuwa moja wa viongozi wa juu wa TOC kukubali mwaliko wa ofisi ya TOC kwa kuja hapa leo  kutufungulia Mkutano huu Mkuu wa Kamisheni ya Wanamichezo.

Ndugu Mgeni Rasmi, ofisi ya TOC imekuwa hapo awali ikialika wageni rasmi hasa katika shughuli hizi za ufunguzi wa mikutano yetu kutoka nje hasa taasisi na serikali, lakini kuanzia sasa itakapobidi shughuli hizi zitafanywa na viongozi wa TOC au Vyama/Mashirikisho ya Michezo.

Ndugu Mgeni Rasmi, tangu Kamisheni ya Taifa ilipoundwa hapo mwaka 2006, kazi kubwa ilikuwa kuhamasisha na kutoa wito kwa Vyama/Mashirikisho ya Michezo kuanzisha Kamisheni ya wachezaji katika Vyama/Mashirikisho yao ya Michezo. Ni Vyama/Mashirikisho chache ambayo yameitikia wito wetu kwa kufanya uchaguzi halali wa kidemokrasia.
Vyama vingi mpaka sasa vimekuwa vikiteua wajumbe wake kuhudhuria Mikutano Mikuu ya Kamisheni inayoandaliwa na TOC, lakini cha kushangaza kwa utafiti ulioofanywa na TOC/KAWATA Taifa, wachezaji hao siyo wajumbe katika Kamati za Utendaji na Mikutano Mikuu ya Vyama na Mashirikisho husika kama Muongozo wa Kamisheni unavyosema.

Sijui ni kwa nini Vyama/Mashirikisho ya Michezo yaogope kuwaingiza wachezaji kwenye chombo cha maamuzi (Kamati ya Utendaji/Mkutano Mkuu). Kuna siri gani kubwa katika vikao vya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu ambayo hayapaswi wachezaji kufahamu? 

Mimi nina imani kabisa wawakilishi wa wachezaji watakapokuwa kwenye vyombo hivyo vya maamuzi malalamiko na manung’uniko mengi ya wachezaji hayatakwepo, kwani watakuwa wameshiriki kikamilifu katika maamuzi.

Mahali ambako Mkutano Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji (Kawata) unapofanyikia leo Zanzibar.
Ndugu Mgeni rasmi, Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC), Vyama/Mashirikisho ya Kimataifa (IFs), ANOCA na NOCs kama TOC  zina Kamisheni zao ya Wanamichezo ambazo kazi zao kubwa ni kama:

1.     Kutoa ushauri, nasaha kwa wanamichezo waliostaafu na ambao bado wanaendelea na michezo.
2.     Kulinda maslahi ya wanamichezo ndani ya maadili ya Olimpiki.
3.     Kutoa mapendekezo kwa mambo yanayohusu maslahi ya wanamichezo ndani ya vikao ya Kamisheni husika.
4.     Kufanya lolote lile ambalo ni kwa faida ya wanamichezo kwa ujumla wake.

Kamisheni yetu ya Kitaifa tangu ianzishwe mwaka 2006 na wajumbe wake Kitaifa kuchaguliwa tena mwaka 2012 mjini Dodoma  imechelewa kwa kiasi fulani kutokana na sababu ambazo ni pamoja na kukwamishwa na viongozi wa Vyama/Mashirikisho yao Kitaifa (NFs).

Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kawaita mjini Zanzibar leo Alhamisi.
Wanamichezo wana uwezo mkubwa wa kushauri viongozi wa vyama/mashirikisho yao katika masuala yanayohusu maendeleo ya michezo, pia kushauri mashirika mbalimbali kuhusu ajira za wanamichezo pamoja na hali ya baadaye mchezaji mhusika anapostaafu.

Mhe. Mgeni Rasmi, michezo kwa sasa ni ajira, ndiyo maana IOC imehamasisha NOCs kuunda Kamisheni za Wanamichezo ili watambuliwe kuwa sekta muhimu ya maendeleo ya michezo katika Taifa letu.

TOC  inaamini kwamba kukiwa na uwakilishi wa wanamichezo katika vyama/mashirikisho ya michezo na asasi za umma nchi yetu itakuwa imepiga hatua katika kupiga vita madawa ya kuongeza nguvu katika michezo ambayo kwa sasa yamepamba moto duniani.
Baadhi ya waalikwa katika mkutano Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania (Kawata) Kutoka kushoto Irine Mwasanga, Peter Mwita na Mwinga Mwanjala wakati wa mkutano huo leo Zanzibar.
Mhe. Mgeni Rasmi, bado vyama/mashirikisho ya michezo ya kutothibitisho yanaendelea. Mwaka huu kutoka Bara ni Vyama/Mashirikisho ya Kuogelea, Mpira wa Magongo na kwa Zanzibar Mpira wa Meza na Kikapu havikuthibitisha, lakini wakatma washiriki. Riadha Tanzania kuwasilishwa na wajumbe 3 (wm 2, mk 1).

Kwa haya machache naomba nikukaribishe ili uzungumze na wanamichezo walio mbele yako kisha utufungulie Mkutano huu wa Kamisheni ya wanamichezo kwa mwaka 2015 kama tulivyokuomba.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.




Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi akifuatilia jambo na mjumbe wa Kamati ya TOC Irine Mashanga wakati wa Mkutani Mkuu wa Kawata Zanzibar .
 



Katibu msaidizi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Jamal Adi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kamishenu ya Wachezai (Kawata) Zanzibar. Kulia kwa Adi ni Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi.

HOTUBA YA MGENI RASMI WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA KAMISHENI YA WACHEZAJI TANZANIA (KAWATA) ULIOFANYIKA ,ZANZIBAR

December 31, 2015
TOC


 
Ndugu Gulam A. Rashid, Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania,

Ndugu Filbert Bayi  Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania,

Ndugu Viongozi wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania,

Wageni Waalikwa,

Mabibina Mabwana.

Awali ya yote, napenda kutoa shukrani zangu kwa viongozi wenzangu wa TOC
kwa kunishirikisha na kunipa heshimahiiyakuwamgenirasmiwakuufunguaMkutanohuumuhimuwaKamisheniyaWachezaji Tanzania.

Kwanza naipongezaofisiyetuyaKamatiyaOlimpiki Tanzania kwakutekelezamaagizoyaKamatiyaOlimpikiyaKimataifayakuzitakaKamatizaOlimpikizaKitaifakujumuishawachezajikwenyeKamatizakezaUtendaji, naMikutanoMikuuyakehalikadhalikanaVyama/MashirikishoyaMichezowanachamawa TOC ambaomichezoyaoipokwenyeratibayaMichezoyaOlimpiki(Summer/Winter).

Ni matumainiyanguwengiwawawakilishiwaliohapaniwajumbehalaliwaliochaguliwanawachezajiwenzaondaniyaVyama/Mashirikishoyamchezohusikakwanjiayademokrasianasiyokuteuliwanaviongoziwavyama/mashirikishoyamichezoyenu, vile vilekutokaamadarakanizaidiyamudawauongoziambaoukokwenyemwongozowenukamamlivyoelekezwanaKamatiyaOlimpikiyaKimataifa (IOC) kupitiaKamatiyaOlimpikiyaTanznaia (TOC).

NatoawitokwaviongoziwaKamisheniyaWachezajiwanaowakilishavyama/mashirikishoyamichezokusaidiananaviongoziwaVyama/Mashirikishohusikailikamahavipohai, basiwajitahidikuvifufuakwamaanayakufanyauchaguzikwamudamuafakakufuatakatibazao. Kuna michezominginehufakutokananakutokuweponamsukumokutokawadauwavyama /mashirikishoyamichezoambaoniwachezaji. ViongoziwaKamishenikatikavyama/mashirikishovinawajibuwakusaidiamaendeleoyamichezokatikataifaletukupitiavyamanamashirikishoyao. Kamishenizilizochaguliwanazilizopoziwezekutoachangamotoyaushauriwanamnayakuendeshamichezonchini, kwanihadiduzarejeazakazizaonipamojanakuamshaariyawachezajiwenginewakitaifanakimataifakatikakufikiamahalipazuri pa kupatawachezajiwatakaowakilishavilabu, vyamanamashirikishoyetukatikangazimbalimbalizamashindano.KAWATA kuanziangaziyaVyama/MashrikishoyaMichezohadiTaifahaziwezikukwepalawamawakatitimuzetuzinapofanyavibayakatikaMashindanoyaKimataifa.

Nimefahamishwakuwawachezajiwengipamojanakwambammekamilikahapakuhudhuriamkutanohuu, lakinindaniyavyama/mashirikishoyenuhampewinafasiyakuwamojawawajumbewaKamatizaUtendajizaVyama, MashirikishonaVilabuvyamichezonakuwananafasiyauwakilishiwenyekurakatikaMikutanoMikuu.Ndaniyanafasihizokunamaamuzimengineyanawahusuwachezajiambaondiyowadauwakubwawavyombovyetuvyamichezohapanchini, lakinimaamuzihayoyamekuwayakiamuliwanaviongoziwavyama/mashirikishoyamichezo,ndiyomaanaTOC naIOC wakalionahilinakuamuawawepowawakilishiwaWachezaji. Ni matumainiyangukamamojawaviongoziwa TOC,VyamanaMashirikishoyaMichezo Tanzania Bara na Zanzibar wametekelezamaagizoya IOC kwafaidayaMichezokatikanchiyetu. .
  
Viongozi wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania Kawata), Katib u Mkuu Amina Ahmed (kushoto) na mwenyekiti wake, Ramadhabi Zimbwe pamoa na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kawata leo Zanzibar.
Binafsi, ninaungakabisaumuhimuwaKamisheniyaWachezajikatika TOC, Vyama/MashirikishonaVilabuvyaMichezo, huuniuamuzimzuriwaKamatiyaOlimpiki Tanzania (TOC)naKamatiyaOlimpikiyaKimataifa (IOC), nanikatikakukamilishaazmayamaadiliyaOlimpikihasakuwapawachezajihakiyakutoamawazoyaokatikaKamatizaUtendajizaVyama/Mashirikishona TOC. 


PiaKamishenikupitiaVyama/MashirikishoyetuyaMichezoipingekwanguvuzoteutumiajiwamadawayakuongezanguvukatikamichezoambakokwasasaumeongezekakwakasi.Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) imeshaanzakupambanananchiambazowanariadha wake wamekuwawakitumiamadawayakuongezanguvukatikariadha.

KamisheniivihamasisheVilabunaVyamavyaMichezokuwanaKamishenizaoilizisaidiemaendeleoyamichezohapanchini, msikubalidaimakutumwakatikamikutanokamahiikwakuteuliwabilakuchaguliwa.

KwahayamachachesasanikotayarikufunguarasmiMkutanowenunakuwatakiakila la kheri.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.
 
Baadhi ya wajumbe wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania (Kawata) wakiwa katika mkutano mkuu wao leo Zanzibar.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu ndiye mgeni rasmi tamasha la michezo la mwaka huu la Karatu

December 31, 2015
TOC

Baadhi ya wanariadha nyota wa kike wakichuana katika mbio za kilometa tano za Karatu mwaka jana

Na Mwandishi Wetu
MKUU wa wilaya ya Karatu, Omary Kwaanq anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa tamasha la michezo la Karatu Jumamosi Desemba 19 kwenye Uwanja wa Mazingira Bora, imeelezwa.

Mratibu wa tamasha hilo, ambalo hufanyika kila mwaka mjini Karatu, Meta Petro alisema kuwa, mkuu huyo wa wilaya ndiye atakayetoa zawadi kwa washindi wa michezo mbalimbali katika tamasha hilo.

Baadhi ya waratibu wa mbio hizo wakijadili mambo wakati wa mbio za mwaka jana.
Alisema kuwa mbali na riadha, ambayo itashindaniwa katika mbio za kilometa 10, tano na 2.5, pia kutakuwa na michezo ya mpira wa wavu, soka, mbio za baiskeli na burudani za kwaya na ngoma.

Akizungumzia riadha, Petro ambaye aliwahi kuwa mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania katika miaka ya nyuma alisema kuwa, wanariadha kibao nyota wamethibitisha kushiriki tamasha hilo katika mbio za kilometa 10 na tano, kwa wanaume na wanawake.
Wanariadha wa mbio za kilometa 10 za tamasha la Karatu wakijiandaa kuanza mbio za mwaka jana.
Aliwataja baadhi ya nyota waliothibitisha kushiriki mbio hizo kuwa ni pamoja na Fabian Nelson, bingwa wa mwaka huu wa Ngorongoro Marathoni Joseph Teophilo, bingwa wa Kilimanjaro Marathoni kwa wanawake, Abiola William na Bazil John.

Alisema kuwa mchezo wa soka ulianza leo Jumatano hatua ya wilaya, ambapo mshindi wa leo atacheza Ijumaa na mshindi wa kesho katika hatua ya fainali, ambapo mshindi ndiye atakuwa bingwa wa mwaka huu katika soka.
Mshindi wa mbio za kilometa tano kwa wanawake, Failuna Abdi akipewa zawadi na rais wazamani wa Riadha Tanzania, Francis John. anayeshuhudia ni mratibu wa mbio hizo, Meta Petro.
 Mbali na riadha na soka, mchezo wa mbio za baiskeli ambao huwa na msisimko wa aina yake,wenyewe utashindanisha washiriki katika umbali wa kilometa 60 kwa upande wa wanawake na wanaume.
Muandaaji wa tamasha la michezo la Karatu, Filbert Bayi (katikati), akiwa na washindi baada ya kukabidhiwa zawadi zao katika tamasha la mwaka jana mjini Karatu.

Tamasha la 14 la michezo na utamaduni la Karatu lilivyong'ara mwaka huu

December 31, 2015
TOC



Na Cosmas Mlekani, Karatu
TAMASHA la 14 la Michezo na Utamaduni la Karatu lilimaliziki mwishoni mwa wiki, huku likifungwa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Omary Kwaanq.
Mbali na riadha, tamasha hilo ambalo hufanyika Desemba kila mwaka, linashirikisha michezo ya soka, mpira wa wavu, mbio za baiskeli na ngoma za utamaduni pamoja na kwaya.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Omary Kwaanq (kulia), akienda kuanzisha mbio za kilomita 10 za Karatu. Kushoto ni mratibu wa tamasha hilo la michezo, Meta Petro na nyuma ni rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Gulam Rashid.
Tamasha lengo kuu la tamasha hilo ni kuibua na kuendeleza vipaji kwa watoto na vijana wa Karatu na vitongoji vyake na Tanzania kwa ujumla ili kuwawezesha kutumia michezo hiyo kupata ajira.
Kwa hivi sasa michezo imekuwa ni ajira kubwa sana duniani, hivyo vijana wa Tanzania pia wanatakiwa kutumia fursa hizo kujipatia ajira kama wenzao wa nchi zingine kama Kenya, Ethiopia na hata nchi zilizoendelea kama Marekani, China na zingine.

 
Timu pia zilichuana katika mpira wa wavu katika tamasha hilo la Michezo la Karatu.
Tamasha hilo lilianzishwa miaka 14 iliyopita na bingwa wa dunia wazamani wa mbio za mita 1500 Filbert Bayi akiwa na lengo la kuibua vipaji katika mchezo wa riadha ili kupata nyota wengine wa mchezo huo hapa nchini, ambao watangara kimataifa kama alivyongara Bayi.
Kama inavyoeleweka kuwa maeneo hayo ya Karatu, Mbulu na kwingineko katika mikoa ya Arusha na Manyara kuna vipaji vingi vya wanariadha kama alivyo Bayi, lakini vinakosa watu wa kuviibua na kuviendeleza, hivyo Bayi kupitia Filbert Bayi Foundation (FBF), aliamua kuanzisha tamasha hilo.
Katibu wa Kamati ya Wanawake ya Kamati ya Olimpiki Tanzania, Nasra Juma akiigagua timu ya Karatu kabla ya kuanza kwa fainali dhidi ya Magereza.
Hatahivyo, miaka ilivyokwenda Bayi aliamua kuongeza baadhi ya michezo pamoja na vikundi vya utamaduni ili kuwaongezea vijana fursa ya kujiajiri.
Michezo iliyofuata baadae ni pamoja na soka, baiskeli, mpira wa wavu na mingine ambayo baadhi yao sasa haichezwi tena kama netiboli.
Nasra akikagua timu ya Magere, ambayo ilifungwa 3-0 katika fainali dhidi ya Karatu.
Kwa upande wa riadha mchezo huo umekuwa na msisimko wa aina yake, ambapo pia umeibua vipaji vya wanariadha wengi nyota ambao sasa wanatamba hata nje ya mipaka kama akina Fabian Joseph, Dickson Marwa, Alphonce Felix na wengineo.
Pia kwa upande wa utamaduni kumekuwa na vikundi kama vya Sangoma Mbulumbulu, ambavyo kwa njia moja au nyingine mbali na kueneza utamaduni pia hutoa ujumbe mahsusi kama ule wa gonjwa hatari la Ukimwi ili kutoa elimu kwa wananchi wa Karatu na vitongoji vyake.



 


Wachezaji wa timu ya Karatu wakishangilia kwa staili ya `Magufuli" (wakipiga pushapu baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Magereza katika mchezo wa fainali.


Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA), Muharami Mchume akikagua moja ya timu za wavu zilishiriki tamasha hilo la michezo la Karatu.







Sekretarieti ya tamasha la Karatu wakiwa kazini kwenye viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu.


Washindi wa kwanza wa baiskeli kwa upande wa wanawake ns wanaume wakiteta baada ya kumaliza mbio hizo za Karatu za kilomita 30 na 60 katika viwanja vya Mazingira Bora Karatu.
 




Usalama ulikuwa wa kutosha katika tamasha la Karatu, ambapo walikuwepo askari wa usalama barabarani, gari la wagonjwa na mgambo ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwa mujibu wa taratibu za mashindano ya kimataifa.
Pikipiki ikiendeshwa na John Mwingereza ikiongoza wanariadha wa mbio za kilomita 10.
Mwenyekiti wa Taasisi ya FBF, filbert Bayi (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Omary Kwaanq wa pili kutoka kushoto) na makamu mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tava), Muharami Mchume kabla ya uzinduzi wa mbio za kilomita 10.

Mary Naali akimaliza wa tatu katika mbio za kilomita tano za wanawake za tamasha la Michezo la Karatu nyuma ya Angelina na Failuna Abdi waliomaliza wa kwanza na pili.
 

Copyright © 2015 - 2025 Athletics Tanzania All Right Reserved

Developed by Gadiola Emanuel
Theme By AP | Developed By Gadiola Emanuel