Lucian na Fabian Joseph Watamba Arusha Tourism Mini - Marathon



  afisa utalii wa tanapa fredy shirima akiwa
anamkabidhi  zawadi  Mwanariadha Reginal Lucian baada  ya kushinda
kilometa 42,baada ya kukimbia kwa muda wa

1:00:05

baadhi ya wanariadha walifanikiwa kupata zawadi katika shindano Arusha tourism Marathon wakiwa katika picha ya pamoja
Na Woinde Shizza,Arusha
Mwanariadha Reginal Lucian  alifanikiwa kushinda kwa upande wa
wanaume,katika shindano la Arusha Tourism Marathon baada ya  kutumia
muda wa 1:00:05,akifuatiwa na mwanariadha wa kimataifa, Fabian Joseph
1:00:14, nafasi ya tatu,Gabriel Gerald muda wa 1.00.37.

katika mashindano hayo ya kilomita 42, yaliyoandaliwa na taasisi la
Alfredo Shahanga na  Mwanariadha kutoka Kenya, Evance Kiblanget
alishika nafasi ya nne baada ya kutumia muda wa 1:07 huku nafasi ya
tano ikishinda  Wilbart Peter na nafasi ya sita akishinda mwanariadha
wa kimataifa Dickson Marwa.

Kwa upande wa wasichana  Angelina Tsere alishinda kwa kutumia musa wa
1:11:17, akifuatiwa na mwanariadha wa kimataifa  Mary Naali muda wa
1:11:23, nafasi ya tatu ulikwenda kwa Mkenya  Ladis Shemayo aliyetumia
muda wa 1:11:37 .

Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa ni ,Afisa Michezo
wa Mkoa wa Arusha,Mwamvita Okeng'o mshindi wa kwanza hadi wa 10
walipewa zawadi.

Viongozi wengine waliotoa zawadi ni pamoja na Katibu Mkuu wa kamati ya
Olimpic Tanzania(TOC), Filbert Bayi, Rais wa zamani wa chama cha
riadha nchini(TAAA)  Franis John na Afisa  Utalii wa TANAPA Fred
Shirima.

Katika mashindano hayo, washindi wa kwanza walipoewa zawadi ta
shilingi 500,000, washindi wa pili, 250,000,washindi wa tatu, 200,000,
wanne 150,000 na wa tano 100,000 ambapo wa 6 hadi 10 pia walipewa
zawadi.

Wakizungumza wakati wa kutoa zawadi, Bayi na Okeng'o walipongeza
wanariadha waliojitokeza kwa kuonesha upinzani mkubwa na kutoa wito
mashindano haya yafanyike kila mwaka ili kusaidia kukuza utalii wa
ndani.

Mkurugenzi wa Alfredo Shahanga kwa upande wake, alisema lengo la
mashindano hayo lilikuwa ni kuhamasisha utalii wa ndani, kuhamasisha
amani mkoa wa Arusha na kutaka sasa riadha itumike kutangaza utalii.

Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya mashindano ya Arusha Tourism
Festival ni mara ya kwanza kufanyika nchini, yalidhamiwa na shirika la
hifadhi za Taifa(TANAPA), kampuni ya vinywaji ya SBC(T) Ltd, Radio
Sunrise,BiG Expedition,Mega Trade Investment,Tanzania Breweries na
Creative Solution.

Post a Comment

0 Comments